Magufuli Afanya Uteuzi Mpya Benki Kuu,,Ateua Manibu Gavana Wawili kwa Mpigo..!!!


Rais John Magufuli jana, Jumatano ameteua manaibu Gavana wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Taarifa ya Ikulu imesema, Rais amemteua, Dk Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha na Dk Bernard Yohana Kibese (Uthibiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha).

Kabla ya uteuzi huo, Dk Kayandabila ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Natu Mwamba aliyememaliza muda wake, alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 Dk Kibese aliyekuwa mtaalamu wa uchumi na fedha wa BoT, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Lila Mkila ambaye amemaliza muda wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad