Magufuli - Barrick ni Wanaume Haswa..Wamekubali,Wametubu na Watalipa Fidia Yetu..!!!


Rais John Pombe Magufuli (JPM) amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni mama ya uchimbaji wa madini ya Barrick Canada, Profesa John Thornton na kufanya naye mazungumzo Ikulu leo.

Amesema Barrick imepitia mapendekezo yote ya kamati ya pili ya mchanga wa madini na kuwa imekubali kulipa chochote ambacho kitaonekana wanatakiwa kulipa.

“Baada ya kuwaona nilifurahi na nikasema hawa ni wanaume, wakasema yaliyotokea ni bahati mbaya na wanatubu kwa hayo.” Amesema

Rais amesema baadaye Barrick watakuja na timu yao ya wanasheria wakati kwa upande wa Tanzania nao itakuwepo timu ya wanasheria wakiongozwa na Profesa  Palamagamba Kabudi.

“Itakuwa ni timu ya maprofesa kwa maprofesa,” amesema.

Amesema timu hiyo ya Barrick ilipitia mapendekezo yote na wakakubali kuwa wapo tayari kulipa baada ya majadiliano na makubaliano yatakayoafikiwa.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bado na boss wa Tanzanigh na almasi nao washuke waje watubu sisi tunataka chetu

    ReplyDelete
  2. Ni wewe JPM ndiye 'mwanaume wa shoka' na tinga-tinga la ukweli........kama sio wewe kuwachimbia mkwara, nani angekuja all-the-way-from-Canada!? MUNGU ATAZIDI KUKULINDA, INSHALLAH.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad