Magufuli Sio Kiongozi, ni Mwanaharakati tu Kama Wengine..!!!


Ukimsikia anavyo lalamika na kuongea kwa uchungu unaweza fikiri ndie Rais aliepewa mzigo mkubwa kuliko wote katika historia ya Tanzania kumbe sivyo kabisa

Kama Rais Ally Hassan Mwinyi angekuwa na 'kipaji cha kulia na kulalamika' kwa uchungu basi sijui ingekuaje.

Mwinyi aliikuta... 
Nchi imefilisika kabisa.
Chakula hakuna mvua hazinyeshi.
wananchi wanapanga foleni kupata unga wa njano wa msaada kutoka USA..
maarufu ugali wa Yanga.
sigara na bia zinaweza kukupeleka polisi.

Nchi ilikuwa hali mbaya mno kutoka Dar hadi Mbeya siku tatu jinsi barabara ilivyo mbovu.

Ruvuma kuja Dar njiani siku tano, huko Lindi na Mtwara ni meli tu hata mabasi hayafiki mishahara ndo kabisa hakuna.Watu kukaa miezi mitatu bila mishahara ni kawaida.

Sabuni hakuna watu hadi wakawa wagunduzi wa majani ya mipapai kufulia
viatu ndo usiseme tunavaa katambuga vipande vya matari ya magari.

Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo lakini Rais Mwinyi hakuwahi hata mara moja.

Kulia kuwa 'kapewa mzigo mzito' wala kumlaumu mtangulizi wake Mwinyi alikuwa 'anatabasam' tu huku anatatua tatizo moja hadi lingine.

Wananchi walikuwa wala hawahamasishwi kumsiikiliza Rais akihutubia, alionyesha 'uongozi' kimya kimya tu hadii mambo yakabadilika.

Sifa ya kiongozi sio kulialia na kulalamika kila mara.Hizo ni sifa za wanaharakati ambao hupenda kuwachota wananchi kwa kuwatia uchungu na kuwaonesha adui wao ambae pengine wala sio adui wao kweli mradi tu 'mhusika ajitoe lawama' ya kushindwa kuja na solution ya matatizo yaliyopo.

Ndo maana wanaharakati wengi hushindwa kabisa kuongoza wakipewa nafasi imetokea mara nyingi wala sio kitu kipya.

Chanzo JF

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad