Mbunge Mwingine CHADEMA Asimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge

Kamati  ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge imependekeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Conchesta Rwamlaza asimamishwe kuhudhuria vikao vitatu vya mkutano wa saba unaoendelea wa Bunge la bajeti baada ya kumtia hatiani kwa kusema uongo.

Julai 11 mwaka jana akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rwamlaza alimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) Profesa Anne Tibaijuka kuwa wakati akiwa Waziri wa wizara hiyo alitumia vibaya madaraka yake.

Rwamlaza alimtuhumu Tibaijuka kwa kujimilikisha zaidi ya ekari 4000 katika Kijiji cha Kyamnyorwa na kwamba kiasi hicho cha ardhi ni zaidi ya kiasi alichoomba kihalali ambacho ni ekari 1098.

Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kauli hizo zilimshushia heshima Profesa Tibaijuka mbele ya Bunge na jamii anayoiongoza.

Pia amesema kauli hiyo zilikuwa zikimgombanisha Profesa Tibaijuka na wananchi wa eneo hilo ambalo lipo ndani ya jimbo lake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad