Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.
Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.
Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.
Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.
Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!
Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.
Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!
Ninawasilisha hoja!
By Ntate Mogolo
Re Road Licence. Mdau alietoa wazo la road license kuwekwa katika mafuta ametoa wazo zuri sana, na badala ya Tsh.50 hata ikitozwa Tsh.25 bado Tija kwa Taifa itakuwepo kubwa tu. Wahusika waupokee ushauri huu
ReplyDeletenampongeza sana aliyetoa mada hiyo kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu.
Deleteuko sawa sana inatakiwa wawe wabunifu
ReplyDelete