Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!

Wanabodi,

Tanzania ni nchi yenye katiba inayoendeshwa kwa misingi ya haki, the rule of law kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni. Kwenye kila jambo linatekelezwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, mahakamani ni mahali pa kutoa haki, tunaomba usiruhusu vyumba na maeneo ya mahakama kutumika kuwa ni sehemu ya udhalilishaji wa watuhumiwa!. Status ya Watuhumiwa wowote mbele ya sheria ni innocent until proven guilt!. Kwa nini watuhumiwa wadhalilishwe tena mbele ya kamera huku wakipigwa picha na video?!.

Tanzania inafuata mfumo wa sheria wa ya Uingereza, common law, ambapo mtuhumiwa huhesabiwa not guilt until proven guilt. Mfumo huu hauruhusu kuwapiga picha watuhumiwa wowote wakiwa mikononi mwa polisi au ndani ya vyumba vya mahakama. Lengo la kuzuia ni ili kuwaepushia watuhumiwa kuhukumiwa na media, "media trial".

Kitendo walichofanyiwa watuhumiwa hawa wawili, Rugemalila na Sing kuchuchumalishwa chini mbele ya camera za waandishi, ni udhalilishaji wa hali ya juu ya haki za watuhumiwa na ni kinyume cha sheria, taratibu na kanuni!.

Lengo la watuhumiwa kuchuchumalishwa, ni wale watuhumiwa wanaoshikwa kwa kufanya fujo, hivyo huchuchumalishwa ili kuwazuia wasitoroke chini ya ulinzi, hivi kweli Rugemalila na umri ule, na Singasinga na unene ule, walikuwa na tishio lolote la kutoroka chini ya ulinzi hadi kuwa chuchumalisha?!.

Sio mara moja au mbili, watuhumiwa wanafolenishwa na kupigwa picha mikononi mwa polisi. Watuhumiwa wanapigwa picha ndani ya vyumba vya mahakama!. Huu ni ukiukwaji wa haki za watuhumiwa!.

Tanzania – Code of Ethical Practice for media photographers and ...

"Contravene laws or lawful orders prohibiting the taking for pictures in the precincts for courts. The law prohibits the taking of pictures of any person (Judges, jurors and witnesses) involved in a proceeding before the court, whether civil or criminal; or to publish any photograph taken in contravention of the order. It could be in the courtroom, in the precincts of the building in which the court is held, or the persons leaving or entering the precincts". 

Kwa msio fahamu, hata watuhumiwa nao ni binadamu na haijalishi wamefanya kosa gani, nao wanastahili heshima na utu wa ubinaadamu wao na sio kudhalilishwa. Watuhumiwa wana haki zao ambao zinapaswa ziheshimiwe.

Hata wahalifu wanaohukumiwa kunyongwa, pia wana haki zao zinazopaswa kuheshimiwa. Mfano mtu aliyehukumiwa kunyongwa mpaka kufa, japo lengo ni afe, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa kwanza daktari ataitwa na kumpima akikutwa na ugonjwa wowote, adhabu ile haitekelezwi hadi atibiwe apone kabisa akiwa fit ndipo anyongwe hadi kufa. Kumnyonga mtu mgojwa ni kumuonea!. Kabla ya kunyongwa viongozi wa dini huitwa kumsalisha sala ya toba, kumuungamisha na kumuombea dua na kama ni Muislamu hutazamishwa kibla ndipo hunyongwa!. Lengo la kueleza haya ni kuonyesha kuwa hata wahalifu wana haki.

Hivyo ni ombi maalum kwa Kaimu Jaji Mkuu wetu, Dr. Ibrahim Juma, tunakuomba please usiruhusu maeneo ya mahakama na vyumba vya mahakama kutumika kama sehemu ya udhalilishaji utu wa watuhumiwa huu unaofanywa wanapokuwa mikononi kwa polisi na ndani ya vyumba vya mahakama zetu!.

Ndani ya vyumba vya mahakama za Uingereza, India na Afrika Kusini, watuhumiwa hawaruhusiwi kupigwa picha wakiwa ndani ya vyumba vya mahakama, au mikononi mwa polisi. Kama sisi tumerithi sheria za Uingereza, kwa nini tuende kinyume cha wenzetu, unless kwa kufanya hivyo, ndio maendeleo yenyewe!.

Kitendo cha kuwapiga picha watuhumiwa ndani ya vyumba vya mahakama, huku kamera za video zikiwamulika, ni kama kuwahukumu kupitia kitu kinachoitwa "media trial", mtu akiishaonyeshwa kwenye TV ni jambazi, hata akijakukutwa hana hatia, mtaani kila apitapo, watu watanyoosheana vidole, "jambazi yule!"

Naamini polisi wanajua kumpiga picha mtuhumiwa mikononi mwa polisi ni kinyume cha kanuni, kumpiga picha mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mahakama ni kinyume cha kanuni, kwa nini haya yanafanyika na tunayanyamazia wakati sheria, taratibu na kanuni zipo wazi?!.

Wanasheria mliopo jf mtatusaidia kwa hili kama tulibadilishwa kutoka kufuata the common law or English Law into American law.

Nimetokea kumfahamu Prof. Ibrahim Juma kwa karibu na sina mashaka kabisa na uadilifu wake katika kutenda haki na kutoa haki ili tuu sio haki itendeke bali pia haki kuonekana imetendeka, "Justice must not only be done but must be seen to be done".

Paskali.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hii mifumo ya kikoloni tunayoifwata ndio maana. Wanakandamizwa walala hoi. Wale wanajiona wasomi wamekuwa kam kikundi cha mabepari wa kuwanyonya walio wengi ambao wapo wapo, muandishi usitetee ujinga, watu tumechoka ukoloni mamboleo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad