Mkishindana na Mimi Nitawaacha - Alikiba

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.


Alikiba anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake.

"Unajua kila binadamu ana tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu yoyote aniingilie kwenye mipango yangu  kwa hiyo ukiwafuata unaweza kujiangusha" alisema Alikiba 

Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu
"Mimi siangalii ushindani na wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na mipango yangu katika muziki" alimalizia Alikiba 
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad