Gambo amesema kuwa wapinzani baadala ya kuanza kupiga porojo zisizo na msingi bali wajipange tu kumsaidia Rais John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano.
"Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoiona mimi serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii, unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia. Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano" alisema Gambo
Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Arusha amesema kuwa kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kutaka kuikwamishan serikali basi watadili naye asubuhi mchana na jioni.
"Kwa mtu yoyote ambaye ataonekana kuikwamisha serikali isitekeleze malengo yake nataka niwahakikishie kwa uwepo wangu hapa tutahangaika naye asubuhi, mchana na usiku kwa mbinu zote zile, kama wanataka porojo wasubiri 2020, sasa hivi kama wanataka tusaidiane kupeleka huduma na maendeleo kwa watu, haiwezekani tukawa na serikali au nchi ambayo kila siku ni porojo tu, kila siku siasa" alisisitiza Mrisho Gambo
Chanzo: EATV
My take:
Kwa kauli hizi, Wakuu wa mikoa na Wilaya wapo kwaajili ya kupoteza upinzani sio kuketa na kusimamia Mendeleo.
Inawezekana vipi mkuu wa mkoa asijue umuhimu wa wapinzani? Sipati picha wajumbe wa nyumba kumi watafanyaje. Wanasiasa wetu hawana elimu ya siasa.
Wnachukulia vyeo kama zawadi na wamesahau cheo ni dhamana. Juzi kati Nape alikuwa anapinga bunge live lakini leo analilia bunge live. Huu ni mfano wa kwamba maisha hupanda na kushuka. Tutende haki bila kumuonea mtu wala kumuogopa Mtu. Acha na yule mkuu wa mkoa anayeharibu shamba la mwanchadema na kuacha shamba la mwanaccm waliyepakana naye.
By figganigga