MZEE Yusuf Afunguka Kuoa Tena Baada ya Mkewe Kufariki Akijifungua

Zikiwa zimepita siku kumi tangu apate pigo la kufiwa na mkewe mdogo, Chiku Khamis, aliyekuwa Mfalme wa Taarab Bongo na Mkurugenzi wa Kundi la Jahazi Modern, Alhaj Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu endapo ataoa mke mwingine.

Mzee Yusuf amefunguka alipoulizwa na Gazeti la Risasi endapo hali yake itarejea kama kawaida, Mzee Yusuf alisema kuwa suala hilo ni la Allah, hivyo akiamua aoe ataoa na kama ameamua kumpunguzia ili atulie, basi atatulia.

“Suala la kuoa tena ni la Allah, nitamuomba kama akiamua mimi nioe nitaoa, kama pengine amenipunguzia ili nitulie basi nitatulia maana hili jambo linatakiwa subira kwa kila kitu, hutakiwi kukurupuka, nikikurupuka nitajikuta nashindwa mtihani huu ambao Allah amenipa,” alisema Mzee Yusuf.

Mke wa Mzee Yusuf, Chiku alifariki Juni 17, mwaka huu katika Hospitali ya Amana alipokuwa akijifungua na kichanga chake na kuzikwa katika Makaburi ya Kisutu, Juni 18, akiwa ameacha watoto wawili wa kike.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Whatta fun uncivilized heartless man you are yaani mkeo amefariki hata mwezi haujaisha tayari kichwabi mwako una ndoto za kuoa mke mwingine najiuliza kama kweli ulikuwa unampenda mkeo kwa dhati toka rohoni mwako au kufariki kwake kwako wewe ni sherehe nini?Kuweni na roho za kibinadamu katika mambo mengine au wewe utaishi milele?Mimi naona ungechukua muda kidogo kufikiria jambo hilo ili kumuenzi mwenzako baadaye ungeyafanya hayo uyakusudiayo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad