Mzee Yusuph Afunguka Kilichosababisha Kuacha Muziki


Mzee Yusuph
Aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ambaye kwa sasa anafahamika kama Alhaj Mzee Yusuph amefunguka kuhusu kuacha kwake muziki na kufanya toba ili kurudi kuwa muumini na kutoa daa’wa.

Akizungumza kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo June 15, 2017 Alhaj Mzee Yusuph amegusia pia jinsi maneno ya watu yalivyofuata baada ya kutangaza na hatimaye kuacha kabisa muziki huku akielezea namna alivyokuwa anakataza watu kwenye Kundi lake wasitende maovu.
“Mimi nimeacha muziki kwa sababu nataka kuwa Muumuni wa Dini ya Kiislamu na kumfuata Mtume Muhammad (SAW). Nilipopata nafasi ya kwenda kuhiji Makka na kushika Al Kaaba nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu.

“Nilipoanza kubadilika nilikuwa nakataza pombe kwenye Band yangu. Siku nisiyowepo walikuwa wanasema Simba leo hayupo. Nilipokuwa nakataza haya mambo wengi walikuwa wakiniambia kwa nini nisifungue Madrasa. Kubadilika kwangu niliachana kwanza na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa maji tu unaposikia kiu.

“Nilizungumza mimi na Mungu wangu nikisema: ‘Wewe ndiye mwenye kutoa msamaha’. Nikafanya show ya mwisho Dodoma nikaachana na muziki. Nilimwambia kwanza mke wangu mdogo mimi nimeacha muziki. Kesho yake nikamuambia mke wangu mkubwa nimeachana na mziki, hawakuamini.” – Alhaj Mzee Yusuph.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad