NAOMBA NIONGEE NA NINYI WAAJIRIWA MNAOMWAMINI MUNGU..!!
Ndugu mpendwa mwajiriwa,
Nakusalimu kwa salamu za kiuchumi.
Sina chai ya kuuza leo, bali ninaenda chapchap kwenye points na kiini cha waraka wangu.
TWENDE...
Naomba unitajie mtu yeyote unaemfahamu katika Biblia kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo ambae alibarikiwa kiuchumi na hakuwa mjasiriamali ama mfanyabiashara. Mtaje tu, nami nikufunulie Biblia na notisi zangu "nikusute" na "umbumbumbu" wako.
Unaniumiza sana ninapoona unasubiri Mungu akubariki kiuchumi, halafu huchukui hatua zozote kujifunza ama kujishughulisha na ujasiriamali ama biashara japo hata kuanza na kidogo ulichonacho. Hilo pepo linalokuaminisha kwamba wewe uliumbwa spesho kwa ajili ya kuajiriwa kiasi kwamba ujasiriamali na biashara unaona havikuhusu, ninalikemea kwa Jina la Yesu, maana ndilo linalomzuia Mungu kukupeleka mbali kiuchumi zaidi ya ulipo.
Tarehe 1 hadi 30, Januari hadi Desemba, unachokumbuka ni kuwahi kazini na kusubiri mshahara, baaaasiiii, halafu unataka Mungu akubariki zaidi kiuchumi. How? Ni kweli unatoa sadaka kwa uaminifu, ni kweli unasali sana, lakini kwa uzembe huo wa kutojiongeza kiujasiriamali, its impossible kwa wewewe kuja siku uwe "financially free". Utamlaumu Mungu kwa kupendelea wengine kumbe shida ni wewe mwenyewe maana Mungu hana upendeleo.
Hiyo bidii uliyonayo kazini ulikoajiriwa laiti ungeielekeza na kwenye kijibiashara japo cha genge tu, sasa hivi (mwaka wako wa saba kazini) ungekua unajenga nyumba yako ya tatu kule Chanika ama Bagamoyo Road. Mfanyakazi unaemwamini Mungu, iwe umeajiriwa serikalini ama private, ukifanya kazi miaka mitano mfululizo, pasipo kufanikiwa kujenga nyumba yako (nzuri) ya kuishi, trust me, unakua ume-under utilize uwezo wa Mungu kukubariki! Wake up! (Rudia mare nne hii paragraph hadi ikuingie kabisa)
Kama unalipwa laki nane kwa mwezi, usitegemee kwenda benki siku moja na kukuta zipo milioni tatu. Hivyo sivyo Mungu anavyobariki, na ukiona hela zilizozidi mshahara wako kwenye akaunti, nenda kazirudishe kwa mwajiri maana watakua wamekosea. Hivi unaelewa kwamba kuongezewa mshahara ama kupandishwa daraja sio mambo yatakayokusaidia kupata uhuru wa kiuchumi?
Hivi unajua kuwa hakunaga mshahara mdogo ama mshahara mkubwa ila ukubwa ama udogo unategemea akili inayoushika mshahara husika? Tatizo sio JPM. By the way kwani kwa JK ulifanya kipi cha maana kwa mshahara wako? Achana na mipigo na posho za kizembe mlizokuwa mnajipatia, maana vingine humo itabidi mkatubu:- hapa naongelea ulichofanyia mshahara wako na marupurupu halali. Utamuonea Magufuli wa watu bure kwamba kafanya maisha yako ya ajira kuwa magumu, kumbe shida ni akili yako na uzembe wako wa kutoji-position vizuri na Mungu ili akubariki kupitia namna unavyoutumia mshahara wako kama mbegu kwenye ishu za ujasiriamali na biashara.
Unalipwa laki sita kwa mwezi then unaniambia mshahara hautoshi. Whaaaaaat????? Hapo hapo kuna mama (tena la saba B) yupo mtaa wa pili anauza mboga gengeni, mtaji wake ni elfu hamsini lakini hadi sasa keshanunua kiwanja na tayari ameshajenga nyumba yake chumba na sebule:- wewe na "lilaki sita lako" na digrii juu, ukifika muda wa kulipa kodi chumba na sebule miezi sita, unatetemeka hadi jasho linafika kwenye nyayo! Kuna shida kubwa kwenye akili yako, sema tu hujajishtukia!
Mie ninakushangaa hadi unaniudhi ujue! Haya yataendelea maishani mwako mpaka lini? Leo kodi tu inakutoa jasho, je siku watoto wako wanne wakiwa English Medium Schools, ada milioni sita kwa term, utafanyaje? Ofcourse najua wengine mko level hiyo ya kusomesha na yanayowapata ni siri yenu na Mungu wenu, maana sio kwa kupaniki huko kila msimu wa ada unapofika!
I CAN SEE "CLEARLY"....
Something is wrong somewhere and you have to fix it haraka sana. Mshahara (even if wawe wanakulipa take home ya milioni nne) will never give you financial freedom my dear. Hebu anza serious kufanyia mambo huo mshahara hata kwa Online Investment au Network Marketing au ujasiriliamali mwingine wowote ili umpe Mungu nafasi ya kukubariki beyond measures. Acha woga, acha kujifanya ama kujisemesha eti ajira imekutinga sana, hebu jitoe sadaka pambana, fanya kitu cha kiujasiriamali. Usidhani ni sifa kusema eti ajira imekubana wakati unaendelea kuteketea kiuchumi.
Hebu acha ujinga bana, haaa! Ninakupenda ndio maana nimekuja kukueleza haya, otherwise ningetulia zangu maskani na wanangu niendelee na mishe zangu.
Kila nilichokuandikia hapa nimekitoa katika Neno la Mungu hata kama sijanukuu moja kwa moja maandiko. Kwa hiyo, naomba usinichukie mimi, na kama una kipaji cha kumaindi watu, basi m-maindi Mungu anaekuwazia mema na alienisukuma nizungumze na wewe kwa niaba yake. Najua huu ni waraka mgumu, so, hata ukiamua kuto-like, sitashangaa, ila ujumbe umefika, au sio? (Jibu hata kimoyo moyo, baaaaasi)
Ni mimi msemaji katika Ufalme wa Mungu,
Idara ya Uchumi.
#SmartMind
Ubarikiwe Mtumishi wa Mungu. Hakika Mungu amekutuma kuniletea ujumbe mimi, asante sana... yaani kama uliniona nilivyokua nimeganda na kam-mshahara tu nikisubiri muujiza
ReplyDeleteAsante kwa waraka huo mtumishi wa Mungu, umeniongezea nguvu zaidi za kuamka kiuchumi. ubarikiwe sana japo sina sadaka.
ReplyDelete