Ndege ya jeshi la NATO imeikaribia ndege ya Urusi iliyokuwa imembeba waziri wa ulinzi wa Urusi lakini ikafukuzwa na ndege ya jeshi la Urusi iliyokuwa ikiisindikiza ndege hiyo.
Vyombo vya habari vilisema kuwa kisa hicho kilitokea katika anga ya kimataifa eneo la Baltic, wakati Sergei Shoigu alikuwa akisafiri kuenda himaya ya Urusi ya Kaliningrad.
Nato baadaye ilisema ilifuatilia ndege za Urusi lakini haakujitambulisha.
Mapema Marekani ilisema kuwa ndege ya jeshi la Urusi iliikaribia ndege ya ujasusi ya Marekani umbali wa mita 1.5.
Lakini Urusi ilisema kuwa ndege hiyo ya ujasusi ilikuwa imefanya uchokozi.
Visa kadhaa kama hivo vimeripotiwa miaka michache iliyopita huku Nato na Urusi wakilaumiana.
Kulingana na mashirika ya habari ya Urusi ndege ya F16 ilipita karibu na ndege ya Shoigu.
Yanasema kuwa kisha ndege ya Urusi ya Su-27, ikaingilia kati na kutoa ishara kuonyesha kuwa ilikuwa imejihami.
Kisha ndege ya Nato ikaondoka.