Ndugai ,awanyooshea Kidole Lowassa, Sumaye kuhusu sakata la Mchanga


Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.

Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.

"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.

Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.

"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesema Ndugai.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ya bunge ni kuwawakilisha wananchi. Wananchi wamedhurumiwa vibaya sana hasa maskini ambao inategemea serikali iwape huduma kuu elimu, hmatibabu,hospitsli. Na haya yanatoka kwenye njia hizi kuu za uchumi kama madini, gas, maji, misiti, ardhi, na mbuga za wanysma kuu zote. Hizi zingesimamiwa na kuongozwa vizuri kama baba Nyerere alivyosema kuwa ni mali za wananchi. Wamekuja kubadili lugha na kuwapa bure, bure, wengine bila hata leseni. Mkiwaacha akina mama wajawazito kuzalia chini, barabarani, wrngi kufa. Watoto wrngi bila mashule, au mashule yasiyo na majengo, wsla viti. Halafu wakuu kama maraisi tuliowspa madaraka ya kutulinfia mali zetu wanatoa bure kwa maraisi nchi za kitajiri tukibadilishana na vimisaada visivyo na tija, .halafu wanatukebei ni maskini, tuashindwa kujiongoza, na watu si sawa nao kwa ajili ya mtu mmoja au wawili ukawakingia kifua. Je, utawashtski vipi hawa watu wa mataifa ukawaacha wahusika wskuu watanzania wsliopotosha umma?. Je kwa nini spika wa bunge ambaye kazi yske kudimamia matatizo ya wananchi yanatatuliwa vizuri kupitia wawakilishi wa wananchi anatia mkwara? Hiki nfivho chombo cha juu. Je wananchi mnaunga mkono. Raisi kasema tuwafuatilie wsliohusika bila kujali chama , cheo wala kabila.
    Namshangaa nfugu waziri kuwakingia kifua maraisi. Hii haileti picha. Wapinzsni ndio mnaowspiga wskiibua hoja sasa hoja iko wazi na Raisi katoa mwongozo mzuri tu. Mnamwambia Lisu pingamizi. Lisu anafuata sheria za kimataifavili zifuatwe. Pingamizi si Lisu.maneno bila sheria ndiyo yanaongoza Tanzania. Lisu anaomba sheria zifuatwe katika kiiongoza nchi na Zitto anaelewa wakati mwingine anacheza. Lakini sheria anazijua.
    Ebu nchi iungane komboeni nchi ifarijike na wote walopotosha wachukuliwe hatuavili mambo haya yasirudie tena. Iwr ni fundisho kwa viongozi wote kwamba unapopata vheo kiwe ni dhamana. Kinahitaji ujasiri, uzalendo, hekima na busara. Na si unfugu, upendeleo na kulindana. Leteni hafhi nchini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad