Nionavyo Mimi, Hakuna Haja ya Uchaguzi wa Urais 2020

Mie ni miongoni mwa Mamilioni ya watanzania ambao tunaamini hakuna haja ya kufanya uchaguzi wa Raisi mwaka 2020, kwani itakuwa ni kupoteza pesa tu.Hatuoni wa kushindana na Magufuli kwenye uraisi kutokana na kasi yake ya kiutendaji.

Hii ni kutokana na Uzalendo mkubwa na maono aliyonayo Muheshimiwa Raisi wetu Dr John P Magufuli. Ni mtu aliyedhamiria kupambana na rushwa, ufisadi, umasikini, maradhi na kukuza uchumi kwa vitendo.

Ndani ya muda mfupi tu ameweza kurejesha morali wa utendaji kazi serikalini kwa slogani yake ya HAPA KAZI TU na pia kufunga mirija ya upotevu wa mapato ya serikali.

HAKIKA ni raisi ambaye Tanzania ILIMUHITAJI. Kufanya uchaguzi wa Uraisi 2020 itakuwa ni kupoteza muda na resources zetu tu, na hakuna haja hiyo! Labda tufanye wa kutafuta madiwani na wabunge tu

Je Wewe Unaonaje Mdau?

By Kansigo From JF

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad