Jengo hilo liliteketea kutokana na kile kilichodaiwa friji bovu, japokuwa kikosi cha zimamoto hakijathibitisha ripoti hiyo.
WATU kadhaa wamethibitika kufariki baada ya moto mkubwa kutokea usiku wa manane katika jengo moja magharibi mwa Jiji la London, Uingereza, ambao unasemekana ulisababishwa na friji mbovu.
Familia zinazokaa katika jengo hilo, zilisikika zikipiga kelele kuomba msaada, wakati wengine wanenasa sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo lenye ghorofa 27 linaloteketea na kutishia kuanguka.
Zaidi ya wakati 600 jengoni humo walijaribu kujiokoa ambapo huduma za magari ya wagonjwa zimesema watu 50 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo.
Habari zaidi zinasema watu walionasa ndani yake walifunga mashuka yao na kuyatumia kama kamba na kujirusha kupitia madirishani ili kujiokoa.
Mashuhuda wamesema waliwaona watu wengine wakiruka kutoka kahtika ghorofa ya 15 ili kujiokoa na wengi wao wakipiga kelele huku vikosi vya waokoaji vikiwatoa wengine katika miali ya moto.
Wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wakiishi katika jengo hilo walijaribu kujiokoa kwa njia mbalimbali.
Tukio hilo la moto limeelezwa kuwa ni kubwa zaidi ambalo halijawahi kutokea jijini London katika miaka ipatayo 30 iliyopita