Rais John Magufuli amesema taasisi yoyote ambayo haitalipa bili za maji, hata kama ni Ikulu ikatiwe maji.
Aliyasema hayo jana Jumatano katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na kusisitiza kuwa miradi ya maji na ulipaji wa bili za maji ni muhimu.
“Mtu asipolipa bili, iwe taasisi yoyote hata kama ni Ikulu, narudia kusema kata,” alisema na kuongeza:
“Kwa sababu tumezoa kudekezana, kwenye mawizara haya nafahamu, fedha za OC na hata fedha za bajeti wanazo, lakini suala la bili ya maji linakuwa si la lazima.”
Alisema unamkuta kiongozi ana faili la kwenda Ulaya, anaenda kwanza Ulaya, ana semina analipa kwanza semina maji anaona si lazima.
“Lakini pale hakuna maji, na wale hawajalipia bili, kwa hiyo fundisho la hapa ni kukata,” alisema.
Alisema hata kama ni hospitali wakatiwe kama hawajalipa kwa sababu wana bajeti.
Alisema kama Mkurugenzi wa wilaya yupo na maji yamekatwa, basi hafai kuwa mkurugenzi.
“ Tukifukuza wakurugenzi kama 10, 20 hivi wale wengine watawahi kwenda kulipa bili za maji,” alisema.
Rais Magufuli: Hata Kama Ikulu Hawajalipa Bili ya Maji, Katani
1
June 22, 2017
Tags
Duh kwa maandishi makubwa"Katani"huku mkimaanisha"Kateni"Mnaudhi kweli jinsi mlivyokuwa mmechemsha kila siku makosa ya kukiandika kiswahili mitandaoni huwa najiuliza kama kweli nyinyi watanzania halisi nikimaanisha mliozaliwa kukuluia na kwenda kwenye shule za kitanzania na kuhitimu hayo masomo yenu ya uandishi jirekebisheni sahihisheni habari zenu mizinguo kabla hamjazirusha mitandaoni watu wazisome mnatutoa stimu
ReplyDelete