Leo Ndio Leo..Rais Magufuli Kukabidhiwa Ripoti ya Pili ya Mchanga wa Madini

John Pombe MAgufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli leo Juni 12, anatarajiwa kupokea taarifa ya Pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Tokeo la picha la magufuli
Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imesema, tukio hilo linatarajiwa kurushwa mubashara kupitia vyombo vyote vya habari zikiwemo Runinga, Redio, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu.
Rais Magufuli alipokea  ripoti ya kwanza ya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini ambao husafirishwa nje ya nchi kwa kutumia makontena, mnamo Mei 24, mwaka huu na baada ya Kamati kuwasilisha taarifa hiyo.

Wachumi na wasomi sanjari na wabunge walitoa maoni tofauti kuhusiana na sakata hilo lililobaini Tanzania hupoteza mabilioni ya fedha kupitia rasilimali zake kutokana na baadhi ya wawekezaji na watumishi wa Umma kutokuwa waaminifu.

Hata hivyo ripoti hiyo ya kwanza ilisababisha Waziri wa nishati na Madini, Pro. Sospeter Muhongo na baadhi ya watendaji wa sekta hiyo kufukuzwa kazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad