Rapper Rosa Ree Aanza Tambo....Adai Msimfananisha na Kina.......

Rapper Rosa Ree Aanza Tambo....Adai Msimfananisha na Kina.......
BAADA ya kutoka kimuziki, msanii wa Hip Hop anayekimbiza na Ngoma ya Up In The Air, Rosary Robert ‘Rosa Ree’ ameanza tambo kwa kusema kuwa hakuna rapa yeyote wa kike anayeweza kufanana au kufananishwa naye hapa Bongo.


Akichonga na Mikito Nusunusu, Rosa Ree ambaye yupo chini ya Lebo ya The Industry inayosimamiwa na Navy Kenzo alisema, kila mwanamuziki ana tofauti yake na hata wanaokuwa wanamfananisha na baadhi ya wasanii wanakuwa wanakosea sana.

“Kuna watu huwa wananifananisha na baadhi ya wasanii wa kike hapa Bongo wanaofanya muziki wa kurap, lakini ukweli ni kwamba nipo tofauti na hao wanaonifananisha nao ambao naona hata kuwataja hapa ni kuwapa kiki kirahisi, kitu ambacho siwezi kufanya kwani hawawezi kufanana nami,” alisema Rosa Ree.


GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad