Msanii Rayuu Afunguka Sababu za Kutokufunga Mwezi Mtukufu

Rayuu
MSANII kutoka Bongo Muvi, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unaomsumbua umemfanya ashindwe kufunga kama alivyokuwa akifanya miaka ya nyuma.

Akizungumza na 3 Tamu, Rayuu amedai kuwa anaumia sana kutotimiza nguzo hiyo muhimu ya dini yake na anafanya kila awezalo kuhakikisha anautibu ugonjwa huo ili siku zijazo aweze kufunga.

“Nimekuwa nikijaribu kufunga lakini kabla siku haijaisha vizuri, vidonda vinatibuka hatari hivyo najikuta nikifungulia njiani, naumia sana kwa hali hii kwani napenda kufunga ila ndo hivyo sina jinsi,” alisema Rayuu

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mola atakukuponya bint.inshaallah...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad