Baada ya kurudi kwenye tasnia ya muziki kupitia wasanii waliotumia vionjo vya nyimbo zake na hivyo kupelekea watu kumkumbuka tena nguli huyu, na yeye ameamua kuingia studio kukumbushia makali yake ya kipindi cha nyuma.
Saida Karoli ambaye amekuwa akiimba nyimbo za asili alitamba sana miaka ya mwanzoni mwa 2000 ambapo waimbo wake ambao ni maarufu zaidi ni Chambua ambao siku za hivi karibuni wasanii kama Darassa, Belle 9, Diamond Platnumz walitumia vionjo vya wimbo huo na kutengeneza nyimbo zao zilizofanya vizuri sana.
Said Karoli ametoa wimbo wake mpya ambao na yeye ametia vionjo vya wasanii hao waliotumia wimbo wake. Wimbo huo una jina asili ambalo kwa kiswahili linamaanisha Maneno Maneno. Usikilize wimbo huo hapa chini;
Sikiliza Wimbo Mpya wa Saida Karoli Aliyochanganya Wimbo wa Diamond na Darassa
0
June 09, 2017
Tags