Shigongo amtolea uvivu Tundu Lissu


Mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Erick Shingongo amemnyoooshea kidole Tundu Lissu na kusema anashindwa kuelewa kwanini Mwanasheria huyo amekuwa ni mpingaji wa mambo mazuri na kusema jambo hili linamshushia heshima.

Erick Shigongo amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema yeye kwanza anapongeza hatua alizochukua Rais Magufuli juu ya sakata la madini na kudai kuwa limekuwa na matokeo chanya kwani kiongozi wa Barrick amelazimika kuja Tanzania na kubembeleza yaishe.
"Namheshimu sana Lissu, sana tu.

Ni msomi wa sheria, tena mzuri tu! Lakini namshangaa, nashindwa kumwelewa kwa kitu kimoja kwamba kwa nini hawezi kukubali pale jambo jema linapofanyika? Mimi nadhani ni kujijengea heshima kubwa sana kuonyesha uzalendo pale nchi inapopambana na wizi wa maliasili ambazo hata hao Acacia wenyewe wameukubali, sasa kwa nini Lissu anaendelea kubeza kile kinachofanyika? Hakika hili linamshushia heshima" alisema Shingongo
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu anamkosoa ndugu Tundu lisu hayupo serious. Viongozi wa siasa jifunzeni kuwa na hadhi safi mnapowakilisha Wananchi. Be serious na si kucheka kama mzaha. Hupozi kwa picha, upo kazini. Lisu anataka hili jambo litiliwe maanani na Watu wajue namna ya kulikabiri na kulizima. Ilibidi waamriwe kufunga mgodi mpaka madai yatimizwe kwanza. ndo mjadala wa pili ufuatwe. kuwanyanganya, hawana leseni.Sielewi mnaongea kama marafiki kwenye business kubwa kama hizi. Hawatawachukulia serious hata. Mnawaita wanakuja mnawakubalia tena kama wao ndo wanye nchi hii.Ni aibu kubwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad