Si Kwa Hii Enzi ya Magufuli...Adai Wanaopata Mimba Mashuleni Hakuna Kuendelea na Shule

Rais John Magufuli amesema wakati wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.

 Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,”amesema.

Amesema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.

“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.

Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza  kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”

 “Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni Wamawake hawa. ambao wanaadhibiwa na wanaume wanaowapa mimba hizi wako huru. Ni wanaume wasomi, wenye madaraka pia na wengine bado wapo masomoni. Kumwadhibu mbinti bila kumwadhibu mwanaume na mara nyingi anakuwa na umri mkubwa kuliko binti ni kumwonea bimti huyu. Na hapa mimi kama mwanamke mwenye binti na kijana sikubaliani nawe raisi wangu. Kwanza wanawake wanasoma kwenye mazingira magumu mno. pili wanawake wengi kielimu tupo nyuma kidogo na sababu kubwa ni mila na desturi zetu zisizobadilika kwenya makabila mbalimbali hapa nchini. Mtoto wa kike kwa makabila mangi ni ndoa, mahali, na watoto. Kama kijakazi. Bado Wanaume hamjautambua bado mchango wa mwanamke kwenye jamii ya leo. Na maendeleo mengi yanashuka sababu ya kutokumthamini mwanamke na kumwelimisha sawa na mwanaume.Wanaume wengi mnatuona sisi wanawake kama chini yenu. tunaona majumbani, serikalini na makazini. Ni wakati umefikia kumthamini mwanamke na kumpa hadhi yake na kumsaidia afikie upeo kimasoma kusudi ajiamini aweze kuwa kila anachotaka kama serikali inamthamini na kumsaidia na kumkingia kifua ili afikie upeo wa juu kielimu.Mchukulie hatua kali huyu mwanaume anayemtunga mimba huyu msichana. Msichana hapati mimba mtini, anatungwa na mwanaume. Je Unajua hii raisi wangu? Mbona upo tu upand mmoja. Unamwadhibu aliyeathirika, utajenga taifa gani la kesho?Kila mwanaume akiacha kumchezea mwanafunzi hakuna mwanafunzi wa kike hata mmoja atakayepata mimba hata. Na kwa sababu unamwadhibu msichana tu hutatatua tatizo la mimba kwa wanafunzi. Nashangaa jinsi unavyochukulia mambo mengine kama mzazi, kama kiongozi wa taifa , hii unawaruhusu Wanaume wafanye watakalo kwa mabinti. Kuna ubakaji mwingi tu. Kata silaha za hawa mabwana.Hapa nitakusifu.Fukuza kazi wafanyakazi wa serikali wanaotembea na wanafunzi. Tunalokuomba sheria zifuatwa. si mwanaume anapelekwa mahakamani anatoa hongo sheria duni ndo tatizo.Addibu mwanaume sawa na mwanamke na tumechoka na uonezi wa kijinsia.Utawala Dume ni upendeleo mkubwa na ni tatizo kubwa Tanzania.Hawa watoto wanahitaji misaada na wanaume adhabu kali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hebu na nyie mjifunze kusema 'NO'...khaa, mtoto wa kike hujui kukataa..!!?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad