CHADEMA walitapelewa sana 2015 - unaweza kuita ni utapeli wa juu kabisa wa kisiasa kuwahi kutokea nchini (the biggest political con in our history); hesabu zao ilikuwa ni kwamba Lowassa angekuja na watu wengi sana na hivyo itawapa uwezo wa kushinda hata mbinu chafu. Jinsi ya watetezi wa ujio wa Lowassa walivyoona wakati ule ni kuwa "Dr. Slaa hachaguliki" lakini Lowassa "anakubalika sana". Hawakuwahi kujiliza Lowassa anakubalika na nani na kwanini.
Na ushahidi unaonesha ni kweli Lowassa alikuja na "kura" nyingi zake kuliko kuja na watu wengi kumfuata hadharani. Walichosahau ni kuwa hawakutegemea kuwa baadhi ya watu wao wenyewe wangewakimbia hasa baada ya move ya Slaa kuondoka.
Ni rahisi kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana watu waliokuwa wamfuata Lowassa "aliko waweko" wengi hawakutegemea kuwa angeenda CHADEMA. Wakati makundi ya vijana yalikuwa tayari kumfuata huko kuna ushahidi mkubwa makundi ya watu wazima na wazee wenye hekima hawakuwa tayari kufanya hivyo hata kama walikuwa tayari "kumpigia kura". Kitendo cha kukosekana watu wengi mashuhuri walioimba "tuna imani na Lowassa" kwenda kumfuata CHADEMA lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa matumaini ya Lowassa ndani ya CHADEMA.
Ndugu zangu, nawahakikishia kama Lowassa angekuja alivyokuja lakini angesema amekuja kumuunga mkono Dr. Slaa katika kugombea Urais leo tungekuwa tunazungumzia mambo mengine kabisa... combination ya Lowassa, Slaa, Mbowe na inawezekana hata Zitto angemuunga mkono Slaa.. CCM wangetegemea zaidi kura zao wenyewe kuliko za wasio wana CCM.
Badala yake, kura za CCM zilimeguka kwenda na Lowassa CHADEMA na wakati huo huo kura za CHADEMA zikamegekuka kwa watu waliomkimbia Lowassa. Hili unaweza kuona kwenye baadhi ya matokeo ya Ubunge ambapo watu walikuwa tayari kumpa kura Mbunge wa CHADEMA lakini kwenye Urais wakampa Magufuli!
Alichofanya Magufuli kiukweli kabisa ni kujiuza yeye mwenyewe na siyo chama chake. Matokeo yake alivuta kura nyingi kwake yeye binafsi na hakuvuta kura nyingi kwa chama chake. Takwimu za uchaguzi zinaonesha wazi trend hii.
Kuelekea 2020 Zitto atakuwa eligible to run. CUF maskini ndio sijui tena maana sioni kupitia CUF nani mwingine baada ya Lipumba na Maalim kuvurugana. Lowassa hata akiamua kugombea tena sidhani kama itakuwa rahisi kivile tena na hasa katika mahali ambapo lile dubwasha a.k.a UKAWA limegeuka UKIWA wa IKAWA halipo tena.
Kwenye uchaguzi ambapo ndani atakuwepo Lowassa, Magufuli, Zitto (je Zitto anaweza kuungana na Lowassa kama Lowassa na Juma Duni Haji?) au mgombea wa chama chake kuna uwezekano kweli wa kuwa na matokeo tofauti?
Ni katika mazingira ya kumsimamisha nani katika upinzani kusimama dhidi ya Magufuli kutokea upinzani?
Lowassa
Lissu
Zitto
Nape (wakitoka/tolewa CCM)
Muhongo (akitoka/tolewa CCM)
Januari (akitoka CCM)
Au tuanze kuzungumzia siasa za 2025? na hii 2020 watu wasalimu amri bila hata kunyanyua mikono kujaribu?
Credit - Mzee Mwanakijiji From jf