TAMKO la Rais Magufuli Juu ya Mimba za Wanafunzi Linapingana na Sheria zilizopo

Tanzania tunayosheria inayoitwa "Statutory Rape"

Sasa hii sheria imewekwa kwa msingi kwamba ukifanya ngono na msichana chini ya miaka 18 - au mwanafunzi kwa ujumla, utakuwa umembaka. Utachukuliwa umembaka kwa kuwa inachukuliwa kwamba katika umri chini ya miaka 18 au kipindi cha uanafunzi, msichana bado ni mtoto na hana akili ya kutambua kwamba kukubali kufanya ngono sio jambo jema. Hivyo huwezi kujitetea kwamba hukumbaka bali mlikubaliana kufanya ngono.

Sasa basi, ikiwa Raisi Magufuli anasema mwanafunzi yeyote akipata mimba asipewe nafasi tena ya kuendelea na shule - kimsingi ni sawa na kusema hakubaliani na sheria ya Statutory Rape.

Kwa maneno mengine - utakuwaje na sheria ya statutory rape - na hapo hapo uamue kwamba mwanafunzi yeyote kupata mimba akiwa shuleni ni uamuzi wake na hivyo moja wapo ya adhabu ni kutompa nafasi ya keundelea na masomo?

Na kumbuka kwamba, kauli ya Raisi Magufuli inadokeza kwamba kila mwanafunzi atakayepata mimba akiwa shuleni kajitakia - yale yale ya kiherehere ya Raisi Kikwete. Hapo hakuna kuangalia sababu wala mazingira ya mimba - awe alibakwa au vinginevyo, mimba ni mimba!

Kwa nini kama Taifa tusijikite katika kuongeza kampeni kuwasaidia hawa watoto kutojiingiza katika ngono za mapema badala ya kutoa adhabu za ujumla zisizoangalia mazingira?

Mie ningemwona Raisi Magufuli ana busara sana kama angesema tutawaruhusu wasome, ila sasa tutatunga sheria atakaempa mimba mwanafunzi afungwe jela maisha! Mimba za wanafunzi zingekoma. Sasa Raisi anaadhibu wanafunzi kuliko wanaowapa mimba!

By Synthesizer/Jamii

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wafungwe"Maisha"Are you jokin'or somethin'?Jus'imagine hiyo adhabu ya life sentence inamkuta mtoto wako mwenyewe aliyezaliwa na mkeo/girlfriend nina uhakika 100% kuwa huwezi kuifurahia hukumu hiyo so please try'n' vitu/mawazo yenye sense rather than nonsense fantasie and selfishness bullshits wish you a wonderful peaceful Iddy

    ReplyDelete
  2. Wewe unayejiita Synthesizer/Jamii acha u bush lawyer wako, Tanzania haina sheria inayoitwa 'statutory rape' hiyo ni sua ya ngapi na ya mwaka gani?sijui umeisoma katika chuo gani labda cha Wagagagigikoko, kama hujui kitu acha kudanganya watu. Eti itungwe sheria atakayempa mimba mwanafunzi afungwe maisha so what, akiwa mwanafunzi mwenzie? acha unywanywa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad