Eric Abidal amesema haamini thamani ya mchezaji Kylian Mbappe imepanda hadi kufika Pauni 120 milioni huku akisema iwapo Barcelona inahitaji kusajili mshambuliaji wajielekeze kwa Osmane Dembele.
Thamani ya mchezaji uyo inaelezwa kupanda kutokana na timu vigogo za Ulaya kumhitaji.
Barcelona imeungana na Real Madrid, Manchester City, Arsenal, Manchester United pamoja na Liverpool kusaka saini ya mchezaji huyo.
Mbappe aliyeisaidia timu yake ya Monaco kutwaa ubingwa wa Ligue 1 msimu ulioisha ameweka rekodi kubwa zaidi ya uhamisho kumng’oa Uwanja wa Stade Louis II.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao 26 katika mashindano iliyoshiriki Monaco.
“Kama tukifikiria kulipa zaidi ya Pauni 100 kama ilivyofanyika kwa Pogba wakati haendani na thamani halisi ya kiwango chake tutajikuta wachezaji wenye vipaji tunawanunua kwa Pauni 200 milioni,” alisema Abidal ambaye amestaafu soka kutokana na matatizo ya moyo.
Abidal alisema ni afadhari Barcelona ikaelekeza nguvu kwa Dembele kwa kuwa walionyesha nia ya kumhitaji tangu mwaka jana.