Tundu Lissu Afunguka" Kumkamata Seth na James Rugemalila ni Sawa Lakini Haitoshi"


Anaandika Mhe: Tundu Lissu
KUMKAMATA HARBINDER SINGH NA JAMES RUGEMALILA NI SAWA LAKINI HAITOSHI!!!! Na Tundu Lissu
Harbinder Singh Seth na James Rugemalila walikuwa ni sehemu muhimu ya mtandao uliokwapua shilingi bilioni 306 zilizokuwa Benki Kuu.
Ni sawa, kwa hiyo, wakifunguliwa mashtaka ya jinai ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, tusije kusahau kwamba walikuwa ni sehemu tu ya mtandao wa ufisadi. Vipande vingine vya chain hiyo viko wapi??? Ili bilioni 306 zitoke Benki Kuu ilikuwa lazima Gavana wa BoT Prof. Benno Ndullu na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Paymaster General, Dr. Servacius Likwelile watoe ridhaa yao.

Gavana Ndullu bado yuko ofisini kama Gavana. Dr. Likwelile ametumbuliwa ili kumpisha mpwa wa Bwana Mkubwa kuwa Katibu Mkuu na Paymaster General.
Ili bilioni 306 zitoke BoT ilikuwa lazima Waziri wa Fedha Saada Mkuya ajue na aridhie. Vinginevyo alikuwa ni Waziri wa Fedha wa aina gani asiyejua jambo kubwa kama hilo ndani ya Wizara yake.

Saada Mkuya sio Waziri wa Fedha tena lakini bado ni mbunge na yuko huru hadi sasa.

Ili bilioni 306 za umma zitoke ilikuwa lazima Rais Jakaya Kikwete afahamu na atoe ridhaa yake.
In fact, ripoti ya Kamati ya PAC ilionyesha ushahidi kwamba Prosper Mbena, wakati huo Msaidizi wa Rais Kikwete na sasa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, aliandika dokezo kwa Gavana Ndullu kwamba Rais ameridhia mabilioni hayo yatoke.
Prosper Mbena sasa ni mheshimiwa mbunge na Kikwete ni mzee ambaye tumeambiwa tusimzungumzie bungeni wala magazetini, tumwache apumzike.

Nje ya hawa niliowataja, wapo wale waliopokea mgawo wa mapato ya udhalimu wa mabilioni hayo.

Wapo waliothibitika kuchukua tuhela twa mboga kama Prof. Anna Tibaijuka na Andrew Chenge (bilioni 1.6 kila mmoja); majaji wa Escrow, watumishi wa serikali na hata wa Ikulu ya Kikwete kama Shabani Gurumo, mapadre na maaskofu, n.k.
Wote hawa ni wahalifu kwa mujibu wa sheria za jinai za nchi hii. Karibu wote bado wako huru na wengine, kama Chenge, wamepanda vyeo na kuwa Mwenyekiti wa Bunge.

Pia kuna taasisi inayoitwa Simba Trust ambayo PAC ilisema inamiliki 50% ya IPTL. Serikali ya Kikwete ilikataa katakata kusema hawa Simba Trust ni akina nani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad