Tundu Lissu Sasa ni "Liability" na Aibu ya Karne Kwa Mawakili Nchini

Ameandika Tundu Lissu kuwa kukamatwa Harbinder Singh Seth na James Rugemalila hakutoshi. Mwanasiasa huyu na mwanasheria huyu kwa sasa anatekeleza mradi maalum ambapo kila hatua inayochukuliwa na Serikali hukurupuka kuipinga.

Alipinga kila kitu Serikali ilipoanza kuchukua hatua dhidi ya uporaji wetu katika raslimali za madini hata pale alipooneshwa kuwa anakipinga alichokipigania hata katika maandiko yake ya nyuma ndio akaishiwa nguvu.

Alianza kupotosha umma kuwa tutashitakiwa lakini alipooneshwa ushahidi kuwa huko MIGA anakotaja vipo vifungu mkataba huo haulindi wezi na watoa rushwa akanywea.

Alipoumbuliwa kuwa alijenga ukaribu wa mashaka na Acacia na upo ushahidi wa nguvu walizompa na wenzake kuropoka na kwamba siku moja utaanikwa na ataanikwa na atapigwa butwaa akanywea.

Sasa amekurupuka kuanza kubeza hatua za mwanzo tu za Serikali kumkamata mfanyabiashara ambaye hata yeye Lissu alitokwa povu huko nyuma kutaka akamatwe.

Mbia wake katika ukaribu na Acacia na kutumika kubeza mambo Zitto Kabwe katika hili amekataa kugeuka jiwe-walau kapongeza juhudi hizi za Serikali.
Lissu anataja majina ya watu weeeengi akisema nao wakamatwe. Sipingani naye lakini mwanasiasa huyu ajue kuwa hoja si kukamata tu hoja kisheria ni ushahidi.

Kesi hizi kubwa ni wazi kuwa Serikali inapambana na watu wenye nguvu na watakaoweka mawakili wengi kuwatetea. Serikali ninavyoiona ina akili kuliko Lissu anavyodhani na ndio maana katika hili nataka kuamini hakuna atakayesalimika hata Lissu mwenyewe.Ipo siku.

Katika sheria kumpeleka mtu mahakamani sio suala la mbwembwe wala kiki za siasa wala hasira bali ushahidi. Lakini kama alivyoropoka mwenywe ushahidi tu hautoshi lazima uwe na ushahidi mzito na wa kuthibitisha kosa husika bila kuacha shaka ya maana (proof beyond reasonable doubt).

Mwanachama mwandamizi wa Chadema na mwalimu wa Lissu katika sheria Prof. Abdallah Saffari ameandika kwa kina dhana hii katika kitabu chake "Mashtaka ya Jinai na Utetezi" Ndio maana naamini hata Prof huyu atakuwa anashangaa ukurupukaji wa Lissu

Ninavyowaona watendaji makini wa JPM wanatimiza kanuni hii ya kisheria na maoni haya ya wasomi watulivu kama Prof. Safari kwa kukusanya ushahidi na wanapoupata wanaoamini unatosha (maana mwisho wa siku Mahakama ndiyo inaamua) ndipo wanakwenda kortini.

Lissu anajua pia kuwa kesi haishindwi kwa mtu kuwahi mahakamani asbh au mchana bali unaishinda pamoja na mambo mengine kuandaa ushahidi kujiridhisha na vifungu vya sheria utakazotumia na mwisho hoja utakazozijenga kortini.

Mimi nakubaliana naye kwamba kuwakamata hawa wawili hakutoshi na wala hata aliowataja hawatoshi na hata Serikali haijasema imetosha! Wapo watu wengi wamelikosea Taifa hili tena wengi Lissu akikwepa kuwataja na baadhi yeye ndio sasa anakuwa wakili wao kuwatetea.

Lipo kundi lililoamua kuhujumu Taifa kwa kuwatumikia mabepari wa nje...hawa nao bado. Nashangaa Lissu hawaoni.Wapo. Wapo wanasiasa ambao huvuta mabilioni kwa watu wanaoliibia Taifa na kuanza kuzuia juhudi za Serikali.Wapo ila Lissu hakuwataja.

Wapo wanasiasa wamekuwa katika kilele cha kashfa kubwa za nchi hii kama vile Richmond Lissu anawajua na yuko nao lakini hakuwataja wala hataki kuona kuwa hao nao bado.

Nilikuwa namkumbusha tu kuwa kama ni dhana ya bado, bado wengi ila aweke orodha yake vyema, asibague.Namhakikishia kwa spidi hii ya kazi wapo pia ambao atakwenda Mahakamani kujaribu kuwatetea.Wapo.Asubiri tu.

Lakini la msingi analopaswa kujua ni kwamba mtu hapelekwi Mahakamani kwa sababu tu kalalamikiwa au katajwa na flani. Ndio maana namuona Lissu kama Rais wa kwanza wa Chama cha Wanasheria Nchini ambaye kwa kweli ni "liability."

Mpaka sasa kaondoka kabisa kwenye kazi hiyo ya kushauri kitaalamu hadi kuwa mropokaji na mtu anayetishia Serikali isichukue hatua au akibeza kila hatua zinapochukuliwa hata katika mambo aliyoyatafiti katika thesis zake na kutaka yafanyiwe kazi.

Ni Rais wa kwanza wa wanasheria ambaye ofisi ya Urais wa TLS imekuwa ya kisiasa rasmi-hana lolote la kuzungumzia taaluma ya sheria wala kujadili utatuzi wa changamoto za taaluma lakini anasubiri Serikali ya JPM iamue kitu tu apayuke.

Ni Rais wa kwanza wa TLS, walau mpaka sasa tangu achaguliwe, huwezi kuona ana vision na mission gani katika kukiongoza chama hicho cha watu makini na wenye utulivu mkubwa. Ni mtazamo wangu kuwa Lissu anaweza kuwa asset lakini so far kwa sasa ni "liability."

Na kwa kweli kwa uliability huo na uasset wa Serikali ya sasa ya JPM, namuona Lissu atakuwa na kazi ngumu sana duniani ya kupayuka na kuna siku atalazimika kujisahau na kupayuka "bado mimi."

Wasalaam
Political Jurist-Udom lakini aliyeko mapumzikoni Nang'ombe, Mtwara
Maramla

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahahahaha!! Hiyo ndio kazi ya wapinzani wa TZ, kupinga tu! Hapo tundulisu anatafuta fursa ya kuwa wakili wao..........wataisoma namba, NA BADO!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad