Tundu Lissu Kuwaponza Lowassa na Sumaye Sakata la Madini

Tundu Lissu Bungeni
Siku moja baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili ya uchunguzi wa makinikia yaliyozuiwa kwenye makontena bandarini na kuagiza viongozi wote walioshiriki katika kulisababishia taifa hasara kupitia sekta ya madini wahojiwe, Wabunge wa upinzani wameibuka na kutaka kinga za marais wastaafu ziondolewe.

Wabunge hao wametaka kinga za Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ziondolewe kupitia marekebisho ya katiba ili nao waweze kushtakiwa kwa kulisababishia taifa hasara ya matrilioni ya fedha kupitia mikataba mibovu ya madini.

Akizungumza jana Bunge, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema kuwa kama serikali imeamua kuwashughulikia wote waliohusika katika sakata la madini, isifanye kwa kubagua badala yake hata marais wastaafu washtakiwe kwani nao ni sehemu ya walioshiriki katika kusainiwa mikataba hiyo.

Wakati wakiyasema hayo, Spika wa Bunge, Job Ndugai (Mb) aliwatahadharisha upinzani kwa kutaka Marais hao washtakiwe kwamba na wao wajue wana Mawaziri Wakuu wawili wastaafu ambao mmoja alihudumu katika serikali ya tatu, na mwengine serikali ya nne.

Mawaziri Wakuu wastaafu walipo katika kambi ya upinzani ni Frederick Sumaye aliyekaa madarakani tangu 1995-2005 chini ya Rais Mzee Mkapa na Edward Lowassa aliyekaa madarakani tangu 2005-2008 alipojiuzulu akiwa chini ya Rais Dkt Kikwete.

Hii ina maana kuwa, kama marekebisho yatafanyika kama ambavyo upinzani wanataka ili kinga ya marais hao iondolewe, ni dhahiri kuwa Lowassa na Sumaye nao watashtakiwa kwani wakati huo ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa shughuli za serikali.

Swali lililobaki kwa watu wengi ni kama upinzani watakuwa tayari kuwatoa kafari wanachama wake hao wawili wakubwa ili wakajibu tuhuma zinazowakabili mahakamani za kusimamia mikataba mibovu wakiwa madaraka. Au, Je! CHADEMA wakijua kuwa mabadiliko ya katiba yatawaathiri pia wanachama wao, Sumaye na Lowassa wataendelea kusisitiza yafanyike?

Jana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Edward Lowassa alisema alipoingia madarakani alikuta kweli mikataba ya madini ni mibovu na alijitahadi kwa kiasi fulani kuirekebisha. Lakini Waziri Mkuu aliyekuwepo kabla yake ni Sumaye, hivyo kwa namna nyingine anasema kuwa Sumaye alisimamia nchi kusaini mikataba mibovu.

Kwa mujibu wa kamati iliyowasilisha ripoti ya uchunguzi mbele ya Rais juzi, ilipendekeza waliokuwa Mawaziri wa Wizara ya Nushati na Madini, Makatibu Wakuu, Wanashaeria Wakuu wa Serikali, Maafisa wa TRA na watumishi wote pamoja na makampuni yaliyoshiriki kuingia mikataba ya madini tangu mwana 1998 wahojiwe, pendekezo ambalo Rais alilikubali.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mkibadili hizo sheria leo ndo zitafanya kazi kwa makosa yaliyopita? (Retrospective), sheria ziko hivyo?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad