Ubuyu wa Moto Moto..Kumbe Ulokole wa Jini Kabula Feki..Anatukana Kila Mtu Anayemuona..!!!


Ubuyu mtamu wa Wikienda! Licha ya mwanamama kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ kutangaza kuachana na mambo ya kidunia na kumrudia muumba wake ‘kuokoka’, ulokole wake unadaiwa kuwa feki.

Ubuyu huo umeibuliwa kutokana na tabia yake ambayo amekuwa akiionesha hasa matumizi ya lugha chafu na matusi ya nguoni anayotoa.

Chanzo makini kilicho karibu na Jini Kabula kilinyetisha ubuyu kuwa, Jini Kabula kwa sasa yupo kama mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia kwani amekuwa akifanya mambo ya ajabu ikiwa ni pamoja na kutukana hovyo katika mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wake wa Instagram.

ANAHITAJI MSAADA WA KISAIKOLOJIA

“Kiukweli Jini Kabula anahitaji msaada wa kisaikolojia maana kinachoonekana yeye mwenyewe hajielewi.

“Siku hizi amebadilika sana, siyo yule wa zamani, aliyetangaza kuokoka kisha akaacha muziki wa kidunia na kudai ataanza kuimba Injili.

“Mambo anayoyafanya Jini Kabula hayaoneshi kuwa na hofu ya Mungu ndani yake maana amekuwa akifanya mambo ambayo hayampendezi

 Mungu wala binadamu, ulokole wake unatia shaka.

“Siku hizi akiamua kuamka na mtu basi utakuta siku nzima ni matusi mitandaoni huku akiweka picha ya muhusika. Inawezekana ametendwa sana katika mapenzi au maisha tu yamemchanganya maana hii siyo bure kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Hivi karibuni Jini Kabula katika ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya bastola na kuwaambia mashabiki wake kwamba atakayechangia vibaya atampiga risasi huku akisindikizia na matusi yasiyoandikika gazetini.

WIKIENDA NA JINI KABULA

Baada ya ubuyu huo kulifikia Wikienda liliingia mzigoni ambapo lilimtafuta Jini Kabula na mazungumzo yakawa hivi;

Wikienda: Jini Kabula umekuwa ukitukana sana watu kwenye mitandao ya kijamii, tatizo ni nini?

Jini Kabula: Piga kimya, utaelewa baadaye.

Wikienda: Kuna habari kwamba una matatizo ya kisaikolojia kwa sababu ya kutendwa sana, hili likoje?

Jini Kabula: Sina matatizo labda hao wanaosema nina matatizo ndiyo wenye matatizo.

Wikienda: Watu wanakushangaa sana kutokana na hilo kwa sababu ulitangaza kuwa umeokoka. Wanajiuliza nini kimetokea?

Jini Kabula: Watashangaa zaidi, wape pole kwa kushangaa.

Wikienda: Wewe unadai ni mlokole, je, huoni kwamba unayoyafanya hayafanani na Mungu anavyoagiza?

Jini Kabula: Kutukana siyo dhambi.

Wikienda: Unasema kutukana siyo dhambi?

Jini Kabula: Titititiii…(akakata simu).

NENO LA MR CHUZ

Baada ya kumsikia Jini Kabula, Wikienda lilimtafuta mzazi mwenzake ambaye pia ni msanii wa filamu, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ambaye alikiri kuchukizwa na tabia hiyo na kwamba alishamkanya mara nyingi, lakini hataki kubadilika.

“Tabia ya Jini Kabula kutukana mitandaoni inaniudhi sana na nilishamkanya mara nyingi. Lakini hanisikii naona ni kwa sababu sina mamlaka juu yake labda mchumba’ke akaye naye na kuzungumza naye ndiye atakayemsikia.”

NENO LA MHARIRI

Jini Kabula kama kweli umeokoka ni vyema ukaakisi matendo ya mtu aliyeokoka na siyo kutumia jina la Mungu vibaya. Ni vyema ukawa moto au baridi na siyo uvuguvugu kwani Mungu hataniwi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad