"Mhe. Magufuli aina ya kiongozi anayestahili kukiongoza Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Hii ni sehemu ya kauli aliyoitoa Prof. Mark Mwandosya mwaka jana akieleza zaidi kwamba hajawahi kuwa hata Mwenyekiti chama ngazi ya shina.
Pamoja na hayo, ni dhahiri Mhe.Magufuli amethubutu kuonyesha nia ya kuondoa ombwe la uongozi serikalini lakini bado haibatilishi ukweli kuhusiana na misimamo tofauti waliyonayo vigogo, washauri na wadau muhimu wa CCM hususani wafanyabiashara wakubwa.
Inasadikika kuwa, CCM Original walibaini mapema kuingiliwa kwa maslahi ya chama na serikali ikiwemo kubanwa kwa wafabiashara ambao ni wafadhili wakubwa wa chama jambo ambalo halisadiki sana Mhe.Magufuli. Hicho ndicho kilikuwa kiini cha Mhe.Chenge kukabidhiwa kiti cha heshima bungeni licha ya kujaa tuhuma rushwa na ufisadi.
Hii ina maana kwamba endapo Mhe. Magufuli atatingisha kibiriti cha chama kinacholindwa na Mtemi Chenge serikali yake itadhibitiwa na Team CCM Original na pengine kupoteza mwelekeo.
Je, Magufuli ataivana na Mhe.Chenge?
Chanzo JF