Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba zinakiuka katiba ambayo wabunge hawa waliapa kuilinda na kuitetea Katiba husika!
Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana wabunge wote huapa kabla ya kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.
Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa kwa kipindi chote cha uwakilishi.
Adhabu za kikanuni za Bunge hazina mamlaka ya kupora wananchi haki zao za kikatiba kama kuwakilishwa.
Kama Mbunge kavunja kanuni Bunge linaweza kumpa faini ili aathirike Mbunge mwenyewe bila kuathiri haki ya kuwakilishwa ya wananchi wa jimbo lake.
Spika Job Ndugai kuwaadhibu askari walioheshimu haki za binadamu pia linatia aibu si kwake tu bali kwa Bunge zima na taifa kwa ujumla.
Chanzo JF
Wanasahau kuwa kukosoa/kukosolewa ni sehemu ya demokrasia kwa sababu mtu hujifunza kutokana na makosa na siyo demokrasia inayoegemea upande mmoja tu hiyo inakuwa ni ugandamizaji wa haki.There are still a lot to be done yaani ni bado sana safari bado ni ndefu sana kuifikia real, fair and true democracy katika nchi nzima na kwa kila raia wa Tanzania.May Lord have a mercy upon us
ReplyDeleteujinga mtupu, walishaonywa mara ngapi???? na alipoombewa msamaha na bunge aliambiwaje????? muwe mna kumbukumbu na matukio siyo kutetea ujinga hawako under 18 ni watu wazima na wanajua wanachokifanya
Delete