Wengi walijua ni mchanga angalau sasa wanajua ni makinikia ambayo baada ya muwekezaji kubanwa alisema ukweli yanamuingizia 50% ya kipato chake chote, Baada ya kubanwa zaidi alisema tangu yazuiwe makontena Kila siku anapoteza Bil 2 za kitanzania. Kabla ya hapo waliaminishwa ni michanga isiyo na cha maana.
Wengine wakisikika kupinga kuwa michanga huwa haisafirishwi wakati miaka yote inapita hapohapo dodoma kuelekea ughaibuni ....
Angalau sasa tunaelekea kufunguliwa bongo nini ni nini katika madini kutoka kwa Serikali, wakosoaji wake,muwekezaji,wachambuzi etc zamani ilikuwa ni malalamiko yasiyoelekea kwenye hitimisho.
Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu
Nguli wa madawa ya kulevya aliyetikisa dunia Pablo Escobar aliwahi kuchoma mahakama, kukodi waasi kufanya mauaji, kufanya Kila unyama ili sheria ya yeye au wauza madawa wenzake wasipelekwe marekani maana kulikuwa na uwezekano 0% kutoroka au kuhonga.
Leo moja ya watuhumiwa wakubwa alihamishwa kutokea gereza la tanzania hadi marekani kitu ambacho huwa ni pigo kubwa kwa mtuhumiwa wa drugs popote ulimwenguni. Pablo Escobar alifananisha na kuwekwa kwenye kaburi la CHUMA(Iron TOMB) yenye uwezekano sufuri wa kutoroka. Yale yaliyokuwa tunadhani hayawezekani sasa yanawezekana.
Asante JPM kwa kufukua Makaburi ya Akili zetu
Ni aibu kupita sehemu kukuta kijiji kinalia njaa huku nyasi zimesitawi mashambani bila kuwepo na zao lolote. Angalau basi pawe na mazao kidogo yaliyokauka kama ushahidi kuwa kuna juhudi zilifanyika lakini mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa kikwazo.
Hapa alionekana katili lkn ukweli ni huo uko dhahiri. Anafungua bongo zetu kuwa kila mtu ajitume kwa kadili ya uwezo wake na akibaki kulalamika basi atakula matunda ya malalamiko yake. Leo ni kawaida kusikia dada mrembo young graduate akiulizia bei ya mbegu za tikiti wakati zamani angekaa sebuleni anaangalia TV hadi muujiza wa ajira utakapomdondokea.
Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu.
Kuna watu walizoea kujenga majumba, kununua magari,kufanya kila aina ya anasa kwa pesa kwa misingi ya rushwa, ujanjaujanja, udaladalali, madilimadili, kukandamiza wasio nacho, dhuruma na uonevu. Angalau sasa kila mmoja anaanza kufikiri upya baada ya mianya hii kuhafifishwa kabisa.
Watu wengi wenye uwezo waliweka akili zao na uwezo wao kando na kujielekeza kwenye njia za mikato zisizohalali ili wanufaike. Leo angalau ni kinyume.
Kila maamuzi yana madhara yake, na wenda matatizo yanayoonekana sasa ktk biashara baada ya muda yatapita tunaamini mambo yatakuwa sawa.
Asante JPM kwa Kufukua Makaburi ya Akili zetu
Nimekuelewa sn...
ReplyDeleteKwa kweli Ahsante nyingiiii tu.
ReplyDelete