Ukweli Usiosemwa..Hali ya Mapato ya Serikali Yashuka, Serikali Haina Pesa Wananchi Tujifunge Mikanda..!!!


Nimepata fursa ya kuongea na kiongozi mmoja toka BOT nilikokuwa nafatilia mambo yangu ya kifedha.

Ni ukweli unafichwa kwa gharama kubwa sana kuwa hari ya kiuchumi wa nchi nimbaya sana.

Mapato ya kodi yameshuka kwa kasi sana na serikali inashindwa kujiendesha vizuri na kuna baadhi ya malipo yamesitishwa hasa kwa wazabuni.

Na njia walio itumia ya kuhamishia makato BOT badala ya hazina ni kuwa kuna baadhi ya taasisi hazitapata fedha kwa wakati hasa makusanyo mbalimbali kama makato ya mishahara na michango mbalimbali kama ile ya mifuko ya hifadhi za jamii, na makato ya hiyari ya taasisi mbalimbali kama vile mikopo nk.

Lengo ni kuzitumia wakati wakikusanya mapato.

Sababu kubwa ya kudorora kwa uchumi inadaiwa ni sera zilizoanzishwa na kupelekea biashara nyingi kufungwa na kuhamisha fedha yoka benki za biashara na kupeleka BOT.

Sasa huko BOT ni vimemo vya maagizo fedha ziende wapi lakni hawafati bajeti pangwa na kujikuta kuwekeza sehemu zisizo na return ya mda mfupi na kuzima mzunguko wa fedha.

Hivyo jamaa kashauri kila pesa unayoipata itunze maana ya kesho haijulikani itakuwaje

Chanzo JF

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad