Duniani kuna mambo mengi sana,na mengine ni mikosi!
Kuna siku nilikuwa nasafiri na gari kutoka kijiji kimoja kwenda kingine. Njiani porini nikamkuta jamaa mmoja anatembea kwa miguu kuelekea uelekeo niliokuwa na kwenda na alikuwa kabeba mfuko we rambo mweusi. Alionekana kachoka sana, nikajua ni sababu ya jua na umbali mrefu.
Nilipotembea kama 10 km, nikafika kijiji alichosema anakwenda, basi nikasimamisha gari. Nikaita "mzee..mzee...tumefika shuka". Akawa kimya. Nikarudia tena, kimya. Kugeuka nyuma ya seat naona mtu kalala. Nikamshika mkono, tingisha kimya. Mungu wangu, nikasema nini tena hii.
Akili ikanijia nimshushe pale barabarani nisepe. Kucheck pembeni nikaona wanakijiji wamekaa. Nikajua hapa noma sasa. Nikamuacha kwenye gari, nikawasha gari na kukimbia kituo cha Polisi. Kufika Polisi na kutoa maelezo, kucheck mtu amefariki. Sitasahau.
Nikawekwa rokapu kwanza kwa siku moja. Kesho yake baada ya uchunguzi, Polisi wakaniambia yule alikuwa mgonjwa na alitoka hospitali kwa daktari kuchekiwa. Na mfuko wake wa rambo ulikuwa na kadi ya hospitali na dawa alizopewa huko hospitali.
Hiyo ikawa pona yangu.
Lakini nilipoteza muda, hela, kuharibu ratiba zangu sana kwa sababu ya kumoa lift mtu nisiyemjua halafu kumbe ni mgonjwa.
Tuwe makini sana.