VIDEO:Tazama Huyu Askari Alivyopinda...Awakamata Boda Boda na Kuwaimbisha Wimbo wa Darasa


Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani lilimewaonya abiria wanaotumia usafiri wa pikipiki maarufu boaboda bila kuvaa kofia ngumu (helmet) kuwa wakikamatwa watakabiliana na mkono wa sheria ambao ni faini au kushtakiwa mahakamani.

Wakati Jeshi la Polisi likitoa onyo hilo kwa abiria, limeeleza kuwa kati ya Juni 5 hadi Juni 14 mwaka huu limekamata pikipiki 2,477 jijini Dar es Salaam pekee kutokana na makosa mbalimbali likiwamo la kupita kwenye taa nyekundu, kubeba abiria zaidi ya mmoja  (mshikaki), kutovaa kofia ngumu na ubovu wa pikipiki zao.

Kati ya pikipiki hizo zilizokamatwa, 1,221 zilikuwa na makosa ya abiria au dereva kutovaa kofia ngumu ambapo abiria 129 walifikishwa mahakamani kwa kosa hilo. Abiria hao walipoachiwa walitakiwa kwenda kununua helmet zao na kurudi kuzionyesha Polisi wakiwa na risiti zao.

Wakati hayo yakiendelea, video moja imesambaa kupitia mitandao ya kijamii ikimuonyesha Afisa wa Jeshi la Polisi akiwaimbisha madereva wa bodaboda wimbo wa Darassa baada ya kuwakamata wakiwa hawajavaa kofia ngumu pamoja na makosa mengine.

Polisi huyo alisema kuwa eneo la Lugalo, Mwenge Dar es Salaam hatopita dereva yeyote ambaye hajavaa kofia ngumu na atakapokamatwa atamshughulikia kisawasawa kwani kwa kufanya hivyo anavunja sheria za usalama barabarani.

Haikufahamika mara moja ni lini video hii ilichukuliwa. Itazame video hapa chini;

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad