Ukarimu wa Vodacom Tanzania Wawafikia Wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo


Vodacom
Kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini Vodacom Tanzania kupitia kampeni yake ya “Ukarimu wa Vodacom” yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku imewafuturisha wakazi wa Kiwanga wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.

Huduma hii yenye lengo la kuendeleza mshikamano inakwenda sambamba na kuwawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla wao kujiunga na kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.

Akizungumza mara baada ya kupata futari, kiongozi wa msafara wa Ukarimu wa Vodacom kanda ya Pwani, Neema Mjuba alisema “Tunashukuru sana tumeshatembelea maeneo tofauti tofauti kanda ya Pwani na Misikiti mbalimbali, tunawashukuru sana wenyeji wetu wa kuweza kutupokea vizuri na kufurahia ofa hii ya ukarimu wa Vodacom”. Zaidi tazama video hapa chini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad