WanaCCM: Tunaburuzwa na Rais Magufuli. Wapinga Uteuzi wa Mghwira..!!!


Rais kuteua wakuu wa mikoa toka vyama vya upinzani alipaswa kupata baraka za chama. Na ikibidi hata kubadilisha vifungu vya katiba ya ccm. 

Nafasi ambazo rais huteua kwa matakwa yake bila ya kufungwa na katiba ya chama chake ni zile nafasi kumi za ubunge. Lakini kamwe siyo ukuu wa mikoa na wilaya. Hawa ni watekelezaji wa ilani ya chama kwa mujibu wa katiba ya ccm. Hivyo wanapaswa kuwa wafuasi ama wanazi wa ccm. 

Huyu rais hana uchungu na chama na ni kwasabb hajawahi kukitumikia chama na hivyo hajui machungu ya kujenga chama. Kuna kila sabb ya kumpinga kwa nguvu zetu zote tutakapokutana ktk vikao vijavyo. 

Haya yanaelezwa kwa uchungu sana na wanaccm, wazee kwa vijana wa sehemu mbalimbali nilikotembelea ili kupata maoni yao kufuatia uteuzi wa m/kiti wa chama cha ACT kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. 

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hamna jipya issue sasa sio chama issue ni umoja wa kitaifa pamoja na maendeleo.Hizo taratibu zimefuatwa sana lakini utendaji bado haulizishi kwa baadhiya wateule.Makonda niwa ccm lakinimbona bado wanampigia kelele.Tusilazimishe watu wafanye vile tunavyotaka sisi.

    ReplyDelete
  2. acha umbea wewe wana ccm gani ulio zungumza nao na wawapi labda wana ccm wa nyumbani kwako wenye akili finyu kama wewe uncle magu yuko sahihi kabisa kwa uteuzi huo kwani wanao tumikiwa iso wana ccm pekee bali watanzania au huyo RC katoka Kenya sio mtanzania ? acha akili mgando wewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad