Watanzania, Tuweke Siasa Pembeni Tumuunge Mkono Raisi Wetu

Rais Magufuli
Wananchi,
Salaam za upendo ziwafikie popote mlipo. Aidha baada ya salaam, nawasilisha mada tajwa hapo juu.
Sintoandika sana kwani, mengi sana yameshaandikwa kwenye nyuzi nyingi sana kuhusiana na suala zima la rasilimali zetu sanasana makinikia(maboso?! ).

Sasa watanzania wenzangu, tunakubaliana kwamba kitendo alichokifanya rais wetu ni kwa ajili ya manufaa yetu. Tumuunge mkono rais kwa vitendo, tuweke siasa na vyama pembeni. Wote kwa pamoja tupaze sauti kupitia maandamano nchi nzima hao mabepari watulipe chetu. Tuache unaa na ujuaji mwingi wa kuandika tuu mitaondi..

Raisi anahitaji msaada wetu kwani hii vita sio rahisi jamani. Pia tumtie moyo huyu kwa hili jema na kubwa alilofanya. Kwa kufanya hivo, tutawapa ujasiri mkuu hata viongozi wanaokuja wa kufanya maamuzi magumu kijasiri zaidi.

Namalizia kwa kusema, hatua aliyofikia raisi wetu pamoja na kamati zote na serikali kwa ujumla ni kubwa ila sio kamilifu kama watanzania tumekaa kimya. Nawahimiza tupige kelele tulipwe na dunia ijue kwamba tupo bega bega na raisi kwa maslahi yetu. Nna hakika mataifa mengine wanatushangaa sana wallahi!

Natoa wito kwa wabunge, madiwani na serikali za mikoa yote tanzania ku-organize maandamano nchi nzima ili ku-support hii move.

Utaifa mbele!
Good morning TZ...

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad