Waziri Lukuvi Kutunukiwa Tuzo ya Uwajibikaji na Utendaji Bora

Viongozi wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na uwajibikaji.

Hayo yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo imedumu kwa muda mrefu.

“Lukuvi ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.

Ameeleza kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu matumizi ya ardhi na umuhimu wake.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona kuwa ni mali.

Mhe. Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao, aliongeza Askofu Mwamalanga.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siyo ukweli wananchi bado tunanyimwa haki zetu za kupewa hati zetu za kumiliki nyumba wakati kila mwaka tunalipa kodi ya majengo na viwanja sasa hapo haki ipo wapi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad