Wizi wa Vipuli vya Magari Dar-es-Salaam na Ukimya wa Polisi na Serikali

Wizi wa Vifaa vya gari
Nimerudi kutoka kazini mida ya saa 12 jioni, nikapaki gari langu ndani ya fence, nikaamua niangalie TV na nakufanya shughuli zangu za ofisini.

Baada ya kula mida ya saa mbili, nikaenda kulala mapema tu.

Naamka hasubuhi, nakuta gari limesogweza karibia na geti na limeibiwa vipuli vya gari, (kuanzia taa za mbele na nyuma, site mirror, bumper la mbele na nyuma, na vitu vya ndani).

Nikaamua kwenda Police kuripoti, nikaambiwa awa watu wako sana na hizi kesi tunazipata kila siku ya mungu, na Police wawili wakakiri ata wao wameshaibiwaga.

Baada ya kuongea na rafiki zangu kuhusu tukio langu, nikaambiwa kitu hichohicho kwamba ata maeneo yeo wamepiga magari kama manne siku za karibuni, na wengine wakinisimulia matukio hayo ya uwizi yalivyowatoke kwao au kwa familia/rafiki zao miezi michache iliyopita.

Kitu kimoja walichokuwa wanaongea sawa na kukubaliana (Police and Raia) ni kwamba wote wanajuwa hivyo vitu vinapopelweka “GEREZANI MNADANI”. Na ata vya kwangu nikaambiwa viko na mpaka wanajuwa vimeibiwa wapi na lini.

Swali langu na natumaini watu wengi wanajiuliza!

Kwa hiyo hii taabia itaendelea mpaka lini? Tunazungumzia vifaa vyenye thamani mpaka zaidi ya million 7 saa nyinginee watu wanaibiwa na visivyopunguwa laki 6.

Hii ni biashara kubwa yenye mtandao mkubwa na inaaribu uchumi wa wananchi wema na kama sio wa Nchi.

Tunashindwa nini kwenda kupafunga Gerezani Mnadani na kuwakamata wausika watoe ushirikiano kuhusu watu wanaofanya uwizi huwo. Kwa ujumla ni eneo linalo ifadhi vitu vya ujambazi, Mpaka wanajigamba kwamba “Si Serikali ya Magufuli wala ya Mtu yeyote itakayoweza kuwafanya kitu”.

Hii ni kauli ya Dharau kwa vyombo vya Dola na Serikali ya Rais wetu Mchapa kazi Magufuli asiyependa watu kama hao wanaotaka kuishi kwa majasho ya watu wengine.

Ombi langu kwa wananchi wenzangu:

Mie nimeanza kupaza sauti , lakini sauti yangu ni ndogo sana, tukishirikiana mimi na wewe hii sauti itakuwa kubwa na itasikika, na Amin’ na waambia RAIS WETU MAGUFULI Hashindwi kuwashughulikia awa watu na hii tabia ikapungua ama kuisha kabisa.

Note: HAKUNA KINACHOSHINDIKANA KATIKA DUNIA.

By Ruukada

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad