KAMPALA: Katikati ya majonzi, yapata siku 15 tu tangu mumewe, Ivan Ssemwaga ‘Ivan Don’ azikwe huko Nakalilo nchini Uganda baada ya kufariki dunia ghafla, aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, anadaiwa kuwatibua Waganda kufuatia kushiriki matukio matano (5) yanayotafsiriwa kuwa ni ya aibu, Amani linayo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya udaku nchini Uganda, tofauti na ilivyotarajiwa, kama ilivyo kwa baadhi ya tamaduni za Kiafrika, kuwa Zari angekuwa kwenye maombolezo kwa siku arobaini au hadi amalize eda kwa kufi wa na mume huyo, yeye amekuwa akijihusisha na ishu ambazo zinaacha watu midomo wazi.
AIBU YA KWANZA
Ilielezwa kwamba, siku mbili tu baada ya mazishi ya Ivan, Mei 30, mwaka huu, Zari alitupia video kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ikimuonesha mwenye furaha tele huku akikata mauno ya hatari hivyo kushangaza wengi walioamini ni video ya zamani.
Ilisemekana kuwa, ili kuonesha video hiyo haikuwa ya zamani, Zari aliambatanisha na maneno yalioonesha alikuwa akijiachia ili kuondoa stresi za majonzi.
Zari ambaye alijirekodi video hiyo akiwa nyumbani kwa mama yake, Halima Hassan huko Munyonyo, Kampala aliandika: “Yote kwa yote ni kujifunza kudensi wakati wa majonzi.”
Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo, wengi walikasirishwa na kitendo hicho huku wakihoji kama ni Zari huyohuyo aliyefi wa na mumewe?
AIBU YA PILI
Achilia mbali kukata mauno, ilielezwa kwamba, tukio linguine la aibu ni pale alipotaka kuzichapa kavukavu na binamu wa Ivan, King Lawrence kwenye kikao cha familia ya jamaa huyo kilichomuhusisha Zari juu ya usimamizi wa mali za baba watoto wake huyo.
Ilidaiwa kuwa, katika tukio hilo, Zari alitia aibu kwa kushindwa kuwaheshimu waliokuwa wakwe zake na kuondoka kwenye kikao hicho kwa hasira akiwa na wanaye watatu wa kiume aliozaa na Ivan, Pinto, Raphael na Quincy.
AIBU YA TATU
Ilielezwa kuwa, tukio lingine la aibu kwa mwanamke huyo ni kitendo cha kushindwa kutulia na watoto hao wa marehemu kwa wakwe zake kasha kukimbilia nao kwao kabla ya kutimka nao nchini Afrika Kusini.
“Alitakiwa akae kwa wakwe au hata kwa mama yake hapa Munyonyo (Kampala) hadi angalau afi kishe arobaini, lakini ametimua na watoto kwa kuwa si mtulivu wala haoni aibu kuwa bado ni mapema kwa mfi wa kama yeye,” kilikaririwa hanzo kimoja na vyombo vya habari vya Uganda.
Hata hivyo, ilidaiwa kwamba, huko Afrika Kusini aliwafanya wanaye hao kuwa katika wakati mgumu kwani badala ya kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoachiwa ya Ivan ambayo watoto hao walikuwa wakiishi awali iliyopo Pretoria nchini Afrika Kusini, yeye aliwapeleka kwa mwanaume mwingine huko Johannesburg ambaye amezaa naye watoto wawili.
AIBU YA NNE
Aibu nyingine anayodaiwa kuifanya Zari katika kipindi hicho kifupi hata kabla ya arobaini ni pamoja na kuvujishwa kwa picha zisizokuwa na maadili zilizomuonesha akijiachia kimalovee na mwanaume mwingine kwenye bwawa la kuogelea.
Taarifa hizo zilieleza kwamba, kama hiyo haitoshi, kilichotibua mambo zaidi hadi kwa jamaa anayeishi naye ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, ni kitendo cha mwanaume huyo aliyekuwa akiogelea naye kumshika sehemu za nyuma za mwili wake ‘msambwanda’ hadharani bila kujali kuwa yupo kwenye kipindi cha majonzi na pia ni mama wa watoto watano.
Katika utetezi wake, Zari alidai kuwa, mwanaume huyo ni binamu wa mumewe na kwamba tukio la uchukuaji wa picha lilifanywa na mke wa jamaa huyo (wifi ye) aliyekuwa akiogelea naye.
AIBU YA TANO
Hata hivyo, ilidaiwa kwamba aibu ya nne ndiyo iliyozaa aibu ya tano kwani Zari alijikuta akiwaporomoshea matusi baadhi ya watu aliodai ndiyo waliosambaza picha za tukio hilo mitandano.
Ilielezwa kwamba, Zari alitumia tusi ambalo haliandikiki gazetini huku akiwaita punda na kuwataka kuacha kufuatilia maisha yake, jambo lililozidi kumtengenezea picha ya tofauti kwa baadhi ya watu wasiomjua tabia zake.
MSAADA WA KISAIKOLOJIA
“Kiukweli nimemfuatilia Zari tangu afi we na aliyekuwa mumewe, hayupo sawa, anahitaji msaada wa kisaikolojia maana anafanya vitu kwa kushindwa kujikontroo,” kilikaririwa chanzo kingine.
Ivan alifariki dunia Mei 25, mwaka huu ambapo tangu hapo kuliibuka mambo mengi hasa juu ya usimamizi wa utajiri mkubwa aliouacha huku Zari akiwa kinara katika mapambano hayo hadi alipoibuka kidedea kwa kumilikishwa sehemu ya utajiri huo ili alee watoto hao watatu aliozaa na Ivan.
Global/Amani