2020:Jee Tundu Lissu Ndiye Asimame na Magufuli?...Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli

Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Jee Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili Magufuli?, sababu mpaka sasa, ndie mwanasiasa wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli!.

Kama kawaida yangu, kwenye kila mijadala yenye kuhusisha maoni ya kisiasa, mimi hupenda kuanza kwa declaration kuwa sina chama, sina kambi na sina upande, kwangu ni maslahi ya taifa mbele.

Baada ya rais Magufuli kuingia madarakani na kuanza na zile tumbua tumbua, nikauliza humu kama kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, jee tuna haja ya kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?,
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

hivyo nikashauri Magufuli aachwe tuu hadi 2025 na ikibidi tubadili katiba aendelee ttuu kama Mkuruzinza, Kagame na Museveni hadi awe kama Mugabe.

Pia kufuatia trend ya chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema kutoonyesha seriousness yoyote kuelekea 2020,
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
nikaconclude kuwa Uchaguzi wa 2020 kwa upande wa urais, litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi kwa ushindi wa walkover kwa CCM.
In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa ...

Lakini kwa mwenendo na matamshi ya Tundu Lissu ya hivi karibuni kumhusu Magufuli, kwa maoni yangu, kwa hapa tulipo, ukimuondoa Zitto ambaye he looks compromised, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani aliyeonyesha uwezo wa kumkabili John Pombe Magufuli kwenye Uchaguzi wa 2020 na Magufuli akapata joto la Uchaguzi.

Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli.

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli huyu huyu jinsi hii hii alivyo ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tuu ndogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, jee akishinda atapewa?.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali/JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. rifungwe tu hili libaba, lisituleteee shida sisi, tunataka maendeleo, stupid man

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad