Kampuni inayomiliki Makampuni ya Uchimbaji wa Madini ya ACACIA imesema italipa mirabaha iliowekwa katika sheria mpya za madini.
Sheria mpya ya madini inawataka wawekezaji katka sekta hiyo kulipa asilimia 6 ya mirabaha ikiwa ni ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali, ambapo asilimia 1 ni kwaajili ya usafirishaji kwenda nje.
Ebu wekeni uwazi makubaliano yote tuyaone. Je Dhahabu kiasi gani wamekichukua. Na hawajalipa kodi kiasi gani. Hakuna kuwapa mkataba tena. Tuonyesheni ngapi watalipa si kwa makinikia tu, kwa dhahabu walizochukua miaka yote hii. Halafu Bunge lijadili namna gani mikataba mipya ianza. Je bado unawaruhusu kuzoa dhahabu Geita? Je huyu makamu raisi Mtanzania ambaye ameshiriki kuficha ukweli. Msichukulie hili jambo juu juu tu. Huu ni mwanzo tu. Ukiona wamerudi ujue wanafaidika sana. Wamesharudisha thamani ya uwekezaji na zaidi. Tunahitaji fifty fifty.Ni hizo papara zenu tena zitatuumiza. Toeni mpango mzima tuuone badala ya kuchukua kitu kidogo tu na majigambo makubwa. Negotiation kama hamhjui unganeni tupate jibu zuri. Hizi cheko za vishido pia ni aibu kama hamtafanya makubwa sasa.
ReplyDelete