Acacia Yalipa Ushuru Milioni 460


Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala, mkoa wa Shinyanga jana Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi hicho.

 “Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.

Alisema kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226 (226,928,115.76/=.

“Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini”,aliongeza Crew.

Katika hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.

 “Mgodi wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.

Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.

“Hiki kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.

Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.

“Sisi tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi Zaidi,” aliongeza Berege
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Migodi ya madini timizeni yaliyomo katika Taarifa ya Kamati mbili za Rais.
    Acheni kung'ang'ania kuuza makinikia au ondokeni maana tumeishawashtukia udanganyifu wenu!
    Hii 0.3% ya ushuru nayo kichekesho!
    Fedha yake haitoshi kujenga hata kilomita moja ya lami!
    Hivi mnapouza madini pamoja na makinikia baada ya tozo zote mnajenga kilomita ngapi!!
    Mwenye mali nusu kilometa nyie kilometa ngapi?!!

    ReplyDelete
  2. Vizuri. Tatizo ni hili. Kwa nini mbapokea shilinhi badsla ya dola. Tunahitaji pesa za kigeni.
    Pili.zilizobaki zitalipwa lini. Ilikuwa dola 190,000,000,000.sasa mnakianika hadharani kiasi kidogo tu bils kusema lini mtapata zilizobaki. Na kwa nini mpokee pesa za madafu.tupeni picha nzima ya madsi tuelewe. Wanapata faida kubwa hawa wstu ndo maana wanabaki. Halafu hata huu mkatsba wa pili si mzuri kwa watanzsnis. Mlipata mwanya ssbsbu ya harskaharska mmekubsli hasara tena. Vichwa maji kwa viongoxi wengi sana. Kufikiri ni mizigo, hslsfu harakaharakaharska na majigambo mengi ssbabu watanzania walio wengi hawaelewi namna gani mikataba ilivyo. Ni woga mtupu badsla ya kujiamini na kudsi haki ambazo ni zenu. Kuna mifano mingi ambayo mngeisngalia mmoja wapo ni nchi ya Botswana ambayo inafaidika sana kwa madini yao.Kuna wabunge wsliwashauti muangslie na muombe msaada huko, watanzania, wanaccm hamkuafiki. Mmeena mmetos tens kws hsrska mkataba mbovu kwa 6% tu
    Na mnapiga kelrle kama nini.ni ndogo sans. Ni nani kati ya viongozi wa juu wa ccm wako nyuma na hili.je hawana maslshi hapa
    ?.Na kama hawana maslahi kwa nini wanarufia tena makosa yaleyyale na asilimia kubwa ya watsnzania wanafurahi. Wazungu wanasema ttTanzania maskini, wanatoa misaada,hivi mpsks leo mnadhindwa kuona hii misaada michahe ndo inayoturudisha nyuma kimaendeleo? Tungrkuwa na skili tukassini mikataba mizuti yenye fsida kwetu. Tukspata haki ambsyo ni yetu. 50% 50% mnajua tusingekuwa maskini sababu seriksli ingejipatis pesa kubwa ya kujiendesha yenyewe. Hslafu hsmngewspigia magoti na kuwabembeleza wawrkezaji ns badsla yske mngewainua watsnzania ns kuwafunfidha ili tukiwekeze wenyewe ns fsida ibski nchini. Au hsmjui kufikiri hivi. Tunamawaziri wengi wasomi, wamesomea mambo ya biashara na uchumi na wanasiass kama akina lipumba ndo kwanza wanagombea vyro vidogo badsla ys kisaifia nchi, kuidhauri vizuri, wanaliliavwawe wsnasiasa pia waihujumu nchi wspatapo vyeo vya juu na hii ni aibu kubwa sana kwa Taifa. Watu wetu wengi wasomi ni mizigo mikubwa nchini.mizigo inayotutia aibu.

    ReplyDelete
  3. Kama walkuwa wanasafirisha UCHAFU kwanini wanalalamika hasara baada ya zuio?

    ReplyDelete
  4. Tusidanganyike wala msitudanganye na kuleta mada ya makanikia. Pesa hii Ni mbizo na wala sisi hatumutanbueni kama akasia . Tunataka kukaa na barrick ili mlipe chetu. Tunawajueni nyinyi magumashi na hii danganya Toto SI katika awamu yetu hii ya tank. Na msitishe kuleta mada ya makanikia. Na kama mnaendelea kukusanya STOPPPPP!!!! Mmetuibia Sana na tunadai Chetu.

    ReplyDelete
  5. AMA kweli...!!!! Ni saws na dola laki mbili na elfu kumi na mbili. Na mkawatoa mitandaoni wamelipa 420M. SI aibu Tu.

    ReplyDelete
  6. Mbona mnabadilisha. SI millioni Ni TRILLIONI 426. TRA WAMESHA WAELEZA. HII INAONESHA NIA YAO SI NZURI NA SI MAAMINIFU WALA WAADILIFU

    ReplyDelete
  7. Mwapachu!! Glaham krew SI aliingia mitini??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad