Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kujiuzulu kwa kushindwa kuwapelekea wakulima wa korosho pembejeo kama alivyoahidi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Katibu wa Itikadi,Mawasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ndg Ado Shaibu amesema kwa sasa bado kuna upungufu wa pembejeo ingawaje serikali ilitangaza kuwa wakulima wa Korosho wangepatiwa bure dawa za kuulia wadudu aina ya Sulpher ili waongeze uzalishaji.
Haibu amesema Serikali iliahidi kupeleka tani 5000 za sulphur lakini imepeleka tani 1500 hali inayosababisha wafanyabiashara kupandisha bei ya mfuko wa sulphur kutoka Tsh 30,000/= hadi 80,000/=.