Msanii wa Bongo Fleva ambaye haishiwi vituko, Harmorapa amekunwa na utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli wa kubana fedha kitu ambacho kimewafanya watanzania kutumia pesa kwa nidhamu.
Harmorapa amesema kipindi hiki cha awamu ya Rais Magufuli kimewafanya watanzania kuithamini pesa ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo na ulazima kitu ambacho ni tofauti kabisa na kipindi cha nyuma.
“Kwanza mimi nimpe tu pongezi kwa sababu amefanya watu wengi sana wajue kuhangaika na wajue kufanya kazi tofauti na kipindi cha nyuma watu walikuwa wazembe”,amesema Harmorapa baada ya kuulizwa swali la kuhoji utendaji kazi wa Rais Magufuli kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM.
Hata hivyo, Harmorapa amesema awamu hii ya tano Serikali imekuwa ikihimiza sana vijana kufanya kazi kuliko kuendekeza starehe kitu ambacho kimewafanya vijana wengi kujituma na kupata molali ya kufanya kazi.
Kijana umeongea ukweli kabisa na hiyo ndio hali halisi ya maisha kama wahenga walivyotangulia kusema ukiona vinaelea ujuwe vimeundwa. Kuwa na kitu ni kiboko ya utu wa mtu na mtu anatakiwa kutengeneza utu wake mwenyewe. Kutegemea mtu kuja kukutengezea utu wako ni moja katika makosa na udhaifu wa hali ya juu kwa mwanaadamu anaejitambua yaani kutegemea mtu mwingine kuja kutengeneza utu wako ni kuuvaa utu wa mtu na hapo ndipo mtu anapoanza kukosa amani na kuanza kumuabudu binaadamu mwenzako badala ya M/MUNGU . Watanzania hasa vijana tunatakiwa kufanya kazi na kufahamu yakwamba hakuna njia ya mkato iliyokuwa salama ya kujipatia kipato. Nchi zote tunazoziona zimepiga hatua na wananchi wake wanatesa kimaisha kwa kuwa na maisha bora walipitia katika hali ngumu sana mpaka kufika pale walipita hali ngumu kuliko inayowakabili watanzania hivi sasa. Kuna nchi zilikuwa jangwa tupu huwezi kuotesha chochote kikaota,maji ya shida kabisa. Tanzania unaweza kuotesha chochote na kikamea. Kuna nchi miaka nenda miaka rudi walikuwa wapo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe Marekani moja ya nchi hizo Tanzania ipo baridi kabisa amani imetawala tangu uhuru. kwa kweli inasikitisha wakati mwengine kuona watu wakilia umasikini Tanzania. Kuna nchi hasa siku za nyuma huko zipo ndani ya barafu karibu mwaka mzima baridi tupu. Tanzania tuna hali ya hewa safi kabisa ya kumuwezesha mtu kufanya kazi mwaka mzima bila ya bughudha. Kwa kweli hali yetu dini Tanzania inasababishwa na uzembe wetu wenyewe . Ndio pale wakati mwengine tunaposema hata M/Mungu atushangaa kutokana na uzembe wetu. Na sasa M/Mungu kajaalia kiongozi alieiona hiyo hali na kuanza kuwahimiza watu kufanya kazi, tayari watu washaanza kumuona adui yaani inakera wakati mwengine fungu la kukosa huwa ni la kukosa ingawa mimi si muumini wa kauli hii ninaamini kila mtu M/Mungu kamuandikia kupata kama mtu huyo atajituma na kufahamu yakwamba kufeli katika jambo ni matayarisho ya M/Mungu kuja kumuwezesha kufanikisha matakwa yako katika hali ya ubora zaidi bali uvumilivu ndio mwelekezo wa M/Mungu na hasira,uvivu,kukata tamaa ni ushauri na maelekezo ya shetani.
ReplyDelete