Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imeshuka kwa asilimia moja ukilinganisha na bei iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.
Kuanzia kesho, bei hizo zitashuka na kuuzwa kwa Sh37 kwa lita (sawa na asilimia 1.81 wakati dizeli itauzwa kwa Sh 14 kwa lita (0.73 asilimia). Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 19 kwa lita (sawa na asilimia 1.03)
Ukilinganisha na bei zilizotangazwa mwezi Juni, nishati hizo zitapungua pia katika bei ya jumla.
Kwa bei za jumla, mafuta ya petroli yamepungua na sasa yanauzwa kwa Sh 37.21 kwa lita(sawa na asilimia 1.92)na dizeli itauzwa kwa Sh 13.70 kwa lita(sawa na asilimia 0.77) na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 18.85 (sawa asilimia 1.10)
Punguzo hilo la bei linatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katka soko la dunia.
Hata hivyo Ewura imetangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga itapanda ukilinganisha na ile iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.
Kwa bei ya rejareja, petroli itapanda kwa Sh 43 kwa lita na dizeli itauzwa kwa Sh 4 kwa lita.
Kwa bei ya jumla, petroli mkoani Tanga imeongezeka na sasa itauzwa kwa Sh 43.07 na dizeli itauzwa Sh 3.81 kwa lita.
Ongezeko la bei ya mafuta kwa mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia kwa shehena iliyoingizwa bandari ya Tanga ukilinganisha na bei ya shehena iliyopokewa Aprili 2017.