Ben Saanane Amezimika Kama Moto wa Kibatari, Nobody Cares. Binadamu Wanasahau Haraka Sana

Nilikuwa mara nyingi sana najaribu kufuatilia maandishi ya mmoja ya waandishi waliopata kutokea kusimamia walichoamini haijalishi kina athari au ukweli kiasi gani. Ben Saanane alikuwa na kitu ana kiamini. Alisimamia hicho. Dunia ya leo ni ngumu sana kupata watu wenye kitu wanachoamini zaidi ya vyeo,madaraka na pesa ni ngumu sana.

Ben Saanane sikuwa nakubaliana na kila alichoandika. kuna mengine nlikuwa napingana naye. lakini nliendelea kumheshimu kuwa alikuwa au ni kijana anayejua kutafuta support na kile anachoamini ili watu wengine pia wapate kukifahamu.

Naamini alikuwa Mwaminifu kwa mtu au watu fulan. Ben Saanane aliishi maisha yake akiamua kuwa mwanasiasa wa Aina yake ambaye hakuwa na jukwaa ambalo angesimama na kuongea kwa kutumia kipaza sauti.

Yeye alitumia kalamu.Iinawezekana kuna infos alikuwa anapewa au ni juhudi yake mwenyewe kuzitafuta. Lakini kinachonifanya leo hii niukumbushe umma habari hizi ni yu wapi Ben Saanane? Jitihada za kumtafuta zimeishia wapi? Je, watu wamekubali kuwa hayupo, amejificha au amepotea?

Tulimtia nguvu, tulimsifu kwa ujasili wake , leo haonekani mbona hatusaidii kumtafuta? hatukumbushi kumtafuta? Je ni kweli kuwa tumeshamwacha apotee?

Kwa namna hii ya usahaulifu, mnadhani tunaweza kuwa na mashujaa siku zijazo? ni nani anajua alipo ben saanane?

By Chizi Maarifa/Jamii Forums
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad