Watu 11 wameuawa kufuatia mashambulio mawili yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na vyanzo vya ndani ya nchi zinasema kuwa watu 5 pia walijeruhiwa katika shambulio lililofanyika mjini Maiduguri.
Vikosi vya usalama viliendelea na operesheni ya kudhibiti hali huku majeruhi wakiwahishwa hospitalini.
Kundi la Boko Haram ambalo lilijitokeza nchini Nigeria mwanzoni mwa miaka ya 2000, lilikuja kuwa tishio na kuanzisha mashambulizi mwaka 2009 baada ya kifo cha kiongozi wao mkuu Muhammad Yusuf ambaye aliwekwa kizuizini.
Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram.