BREAKING News: Polisi wamkamata Halima Mdee nyumbani kwake


Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay saa  moja iliyopita.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza majira ya  saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.

 Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo  kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya  hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole dada, kwa kupigania haki na usawa kielimu.taifa litageuka kwa elimu za juu. Ipo siku.

    ReplyDelete
  2. Usitake kushindana na serikali, utaumia bure........mfyuu, hao wapambe hawakusaidii chochote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad